BENKI ya Biashara ya DCB imesema itaendelea kufanya jitihada tofauti katika kusaidia afya za watanzania wenye uhitaji wa kupata damu kutokana na kukabiliwa na changamoto mbalimbali imeelezwa jijini Dar es Salaam leo.
Akizungumza katika zoezi la kujitolea damu kama sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wachangia Damu Duniani, jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Bw. Sabasaba Moshingi alisema yeye pamoja na baadhi ya wafanyakazi wenzake wameamua kujitolea damu kwani licha ya benki yao kujishughulisha na utoaji wa huduma za kifedha lakini pia wanabeba jukumu la kuhakikisha watu wanaohitaji damu salama mahospitalini wanazipata bila kuwa na haja ya kusubiria ndugu waje kujitolea.
“Leo tupo hapa pamoja na washirika wenzetu hospitali ya Aga Khan kwa lengo la kuchangia damu, tutaendelea kushiriki matukio mengine kama haya na mengineyo yenye lengo la kusaidia kuokoa maisha ya watanzania wenzetu wenye uhitaji wa damu na mahitaji mengine ya kibidamu”, alisema Bw. Moshingi.
Akizungumza katika hafla hiyo Mkuu wa Kitengo cha Maabara katika Hosptali ya Aga Khan, Dk. Caroline Ngimba alitoa hamasa kwa watanzania wote nchini kuwa na moyo na utamaduni wa kujitolea damu bila kusubiri siku rasmi za kitaifa ama kimataifa bali liwe ni jambo endelevu kwani uhitaji wa damu upo kila siku mahospitalini.
“Uzuri ukichangia damu kama afya inaruhusu kila baada ya miezi mitatu unaweza kuchangia tena, tungeomba tabia hii iwe endelevu kwani hakuna kiwanda cha kutengeneza damu, damu inayopewa mwanadamu inatoka kwa mwanadamu”, alisema Dk. Caroline.
Naye mtaalamu wa utoaji damu kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Peter Chami alitoa shukurani kwa Benki ya DCB, huku akizitaka taasisi nyingine kuiga mfano wa benki hiyo ili kuokoa maisha ya watanzania wenye shida ya damu kwani mahitaji ya damu ni makubwa sana.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Bw Sabasaba Moshingi, akifanyiwa uchunguzi wa afya yake kabla hajajitolea damu katika Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam leo, alipongoza baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo kujitolea damu, kuadhimisha Siku ya Wachangiaji Damu Duniani. Picha nyingine zikionesha matukio mbalimbali katika hafla hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...