Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha (wa pili kushoto) na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uwakala wa Vyuo Vikuu Nje ya Nchi (Global Education Link ltd) Bw. Abdulmalik S. Mollel (wa pili kulia) wakisaini hati ya Makubaliano ya Ushirikiano baina ya Taasisi hizo.

*********

Chuo Kikuu Mzumbe kimeingia katika hatua mpya ya kuimarisha ushirikiano wa kitaaluma wa kimataifa kwa kusaini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano na Taasisi ya Uwakala wa Vyuo Vikuu Nje ya Nchi (Global Education Link ltd). Hafla ya utiaji saini huo imefanyika tarehe 23 Juni 2025 katika Makao Makuu ya taasisi hiyo, Jijini Dar es Salaam.

Makubaliano hayo ya kimkakati yanalenga kupanua fursa za elimu ya juu kwa wanafunzi wa Mzumbe na wa kimataifa, kupitia uhamaji wa wanafunzi, ubadilishanaji wa wahadhiri na uwezekano wa kuanzishwa kwa matawi ya Chuo Kikuu Mzumbe katika mataifa mbalimbali pamoja na kupokea matawi ya vyuo vingine vya kimataifa kwa Kampasi za Chuo Kikuu Mzumbe.

Pia, makubaliano haya yataimarisha huduma za mafunzo, kukuza ushirikiano wa kitaaluma na kuimarisha taswira na chapa ya Chuo kimataifa.

Akizungumza katika tukio hilo, Prof. Mwegoha alieleza kuwa ushirikiano huu ni hatua muhimu katika kuandaa wanafunzi wa Mzumbe kwa ushindani wa kimataifa, na kuongeza kuwa unatarajiwa kuleta mageuzi chanya katika sekta ya elimu ya juu nchini Tanzania.

Kwa upande wake, Bw. Mollel alisisitiza dhamira ya Taasisi ya Uwakala wa Vyuo Vikuu Nje ya Nchi kushirikiana kwa karibu na Mzumbe katika kuhakikisha mafanikio ya makubaliano haya yanaonekana kwa vitendo.

Makubaliano haya ni sehemu ya mkakati wa Chuo Kikuu Mzumbe wa kukuza huduma za ukimataifaji na kuimarisha nafasi yake kama taasisi ya elimu ya juu yenye ushindani katika jukwaa la kimataifa.

Hafla hiyo iliongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha na Mtendaji Mkuu wa Global Education Link, Bw. Abdulmalik S. Mollel na kushuhudiwa na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo – Taaluma, Utafiti na Ushauri, Prof. Hawa Tundui Petro, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo – Mipango, Fedha na Utawala, Prof. Allen Mushi Mkurugenzi wa Ukimataifaji na Baraza la Wahitimu, Dkt. Lucy Massoi, Mwanasheria wa Chuo Wakili Masoud Ndwata na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko, Bi. Lulu Mussa pamoja na sehemu ya menejimenti ya Taasisi ya Uwakala wa Vyuo Vikuu Nje ya Nchi.

Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uwakala wa Vyuo Vikuu Nje ya Nchi (Global Education Link ltd), Bw. Abdulmalik S. Mollel akitambulisha timu ya Menejimenti ya Taasisi hiyo na kueleza matarajio na malengo hati ya Makubaliano ya Ushirikiano na Chuo Kikuu Mzumbe. Hafla ya utiaji saini huo imefanyika tarehe 23 Juni 2025 katika Makao Makuu ya taasisi hiyo, Jijini Dar es Salaam. Lengo ikiwa ni kuimarisha huduma za mafunzo na ujifunzaji, kuongeza wigo wa huduma za kielimu pamoja na kuboresha huduma za ukimataifaji na kukuza chapa ya Chuo ndani na nje ya nchi.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha akitambulisha wajumbe kutoka Chuo Kikuu Mzumbe alioambatana nao na kueleza matarajio ya Chuo kwa kukubali kusaini hati ya Makubaliano ya Ushirikiano na Taasisi ya Uwakala wa Vyuo Vikuu Nje ya Nchi (Global Education Link ltd).



Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uwakala wa Vyuo Vikuu Nje ya Nchi (Global Education Link ltd), Bw. Abdulmalik Mollel akiwaonesha na kuwaelezea wajumbe kutoka Chuo Kikuu Mzumbe majukumu na shughuli zinazofanywa na Taasisi hiyo, walipofika ofisini hapo kwa ajili ya kusaini hati ya Makubaliano ya Ushirikiano na Chuo Kikuu Mzumbe.
Mkuu wa mahusiano ya Nje wa Taasisi ya Uwakala wa Vyuo Vikuu Nje ya Nchi (Global Education Link ltd), Bw. Robert Kibona akieleza maono na mchakato wa Taasisi hiyo, mpaka kufikia kusaini hati ya Makubaliano ya Ushirikiano na Chuo Kikuu Mzumbe.
Mkurugenzi wa Ukimataifaji na Baraza la Wahitimu Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Lucy Masoi akieleza maono na mchakato wa kwa upande wa Chuo, mpaka kufikia kusaini hati ya Makubaliano ya Ushirikiaono na Taasisi ya Uwakala wa Vyuo Vikuu Nje ya Nchi (Global Education Link ltd).
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha (wa pili kushoto) akibadilishana hati ya Makubaliano ya Ushirikiano baina ya Taasisi hizo na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uwakala wa Vyuo Vikuu Nje ya Nchi (Global Education Link ltd), Bw. Abdulmalik S. Mollel (wa pili kulia) mara baada ya kusaini hati hizo.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha (kushoto) akimkabidhi zawadi ya kumbukumbu Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uwakala wa Vyuo Vikuu Nje ya Nchi (Global Education Link ltd), Bw. Abdulmalik S. Mollel (kulia) mara baada ya kusaini hati ya Makubaliano ya Ushirikiano baina ya Taasisi hizo.
Picha ya pamoja ya Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha (wa tatu kushoto), Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uwakala wa Vyuo Vikuu Nje ya Nchi (Global Education Link ltd), Bw. Abdulmalik S. Mollel (wa tatu kulia), wajumbe wa menejimenti ya Taasisi hiyo na timu ya Chuo Kikuu Mzumbe mara baada ya kusaini hati ya Makubaliano ya Ushirikiano baina ya taasisi hizo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...