JANA tumeshuhudia kufungwa rasmi kwa msimu wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara 2024/25 kupitia pambano la kusisimua la watani wa jadi, ambapo Yanga SC waliwakaribisha Simba SC katika Uwanja wa Benjamin Mkapa na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0. Ushindi huo umeifanya Yanga kutawazwa kuwa mabingwa wa ligi kwa mara ya 31 katika historia yao. Ligi imemalizika kwa kuwaacha wabashiri wakiwa matajiri haswa wale watumiaji wa meridianbet kwani pesa ilikua ya kutosha kwao.

Mabao ya Yanga yalifungwa na Pacome Zouzoua kwa mkwaju wa penalti na Clement Mzize aliyefunga katika dakika za lala salama. Kwa ushindi huo, Yanga walikusanya pointi 82, wakitangulia Simba waliomaliza nafasi ya pili kwa alama 78.

Msimu wa 2024/25 ulihusisha jumla ya timu 16, kila moja ikicheza michezo 30, nusu nyumbani na nusu ugenini. Timu za Yanga, Simba, Azam FC na Singida Black Stars ndizo zilizomaliza katika nafasi nne za juu, hivyo kujihakikishia ushiriki kwenye mashindano ya kimataifa msimu ujao. Yanga na Simba watashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, huku Azam na Singida wakielekea kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho la CAF.

NB: Jiunge na Meridianbet na ujionee ushindi rahisi kupitia michezo mbalimbali ya kasino ya mtandaoni. Pia unaweza kuongeza kipato chako kwa kubashiri mechi zenye ODDS KUBWA. Piga *149*10# au tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz

Kwa upande mwingine, msimu huu haukukosa machungu kwa baadhi ya timu. Kagera Sugar na Ken Gold zimeshuka daraja moja kwa moja, na kutoa nafasi kwa Mtibwa Sugar na Mbeya City kupanda ligi kuu. Tanzania Prisons na Fountain Gate watalazimika kushiriki michezo ya mtoano dhidi ya Stand United na Geita Gold ili kubaini hatima yao.

Kwenye upande wa takwimu binafsi, mshambuliaji wa Simba, Jean Ahoua, ndiye aliyeibuka kinara wa ufungaji kwa mabao 16, akifuatiwa na Clement Mzize wa Yanga aliyefunga mabao 14. Hat-trick kadhaa zilishuhudiwa msimu huu, ikiwemo ya Prince Dube dhidi ya Mashujaa, Ahoua dhidi ya Pamba Jiji, Steven Mukwala dhidi ya Coastal Union, na Stéphane Aziz Ki dhidi ya KMC. Mchezaji aliyewavutia wengi ni Sowah wa Singida BS, aliyesajiliwa dirisha dogo na kufunga mabao 12 katika michezo 12 tu.

Kwa upande wa makipa, Mousa Camara wa Simba aliweka rekodi ya mechi 19 bila kuruhusu bao (clean sheets), akilingana na rekodi ya Aishi Manula ya msimu wa 2017/18. Hata hivyo, alishindwa kuivunja baada ya kufungwa mabao mawili kwenye mchezo wa mwisho dhidi ya Yanga.

Miongoni mwa matukio ya kukumbukwa msimu huu ni matumizi ya waamuzi wa kigeni kwenye mchezo wa mzungukon wa pili wa Derby ya Kariakoo, jambo ambalo halijazoeleka. Pia kulikuwa na sintofahamu na migomo ya klabu za Simba na Yanga kuhusu baadhi ya mechi, hali iliyosababisha mabadiliko ya uongozi ndani ya Bodi ya Ligi.

Katika eneo la ushambuliaji, Yanga iliongoza kwa kufunga mabao 83, ikifuatiwa na Simba waliopachika 69. Kwa upande mwingine, timu za Pamba Jiji, Kagera Sugar na Ken Gold zilisuasua kwenye safu ya ushambuliaji, kila moja ikiwa na jumla ya mabao 22.

Kwa safu ya ulinzi, Yanga pia walijipambanua kwa uimara wao baada ya kuruhusu mabao 10 tu msimu mzima, wakifuatiwa na Simba (13) na Azam (19). Ken Gold na Fountain Gate ndizo zilitajwa kuwa na safu dhaifu zaidi za ulinzi baada ya kuruhusu mabao 62 na 58.

Ingawa ligi kuu imetamatika lakini bado una fursa kubwa ya kufanya bashiri zako kupitia meridianbet kwani michezo mingi bado inaendelea. Jisajili sasa na uanze safari yako ya ubashiri.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...