Songea, Ruvuma.

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini Dkt. Damas Ndumbaro, leo Juni 30, 2025, amechukua rasmi fomu ya kuwania tena nafasi hiyo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Tukio hilo limefanyika katika ofisi za CCM Songea Mjini ambapo Dkt. Ndumbaro amesema dhamira yake kuu ni kuendeleza juhudi alizoanzisha awali katika kuleta maendeleo ya kweli kwa wakazi wa Manispaa ya Songea.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fomu na Katibu wa CCM Songea Mjini James Mgego, Dkt. Ndumbaro amesema kuwa anaendelea kutekeleza mpango wake wa kuhakikisha Manispaa ya Songea inakuwa Jiji.

Ameeleza kuwa hatua hiyo si tu ni mafanikio ya kiutawala bali pia ni kichocheo muhimu cha maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kimaendeleo kwa wananchi wa jimbo hilo.

Katika muhula wake uliopita, Dkt. Ndumbaro alibainisha kuwa amefanikisha utekelezaji wa miradi kadhaa ya msingi kama vile uboreshaji wa miundombinu, sekta ya elimu, afya na huduma nyingine za kijamii.

Amesema kuwa miradi hiyo ni sehemu ya mpango mpana wa kubadilisha sura ya Songea na kuwa kivutio kikubwa cha uwekezaji, aliongeza kuwa azma yake ni kuhakikisha kuwa miradi hiyo inaendelezwa kwa kasi zaidi katika awamu ijayo.

Aidha, Dkt. Ndumbaro ameahidi kuanzisha miradi mipya ya kiuchumi ikiwemo ujenzi wa viwanda vidogo na vya kati ambavyo vitatoa ajira kwa vijana na kuchochea uchumi wa ndani. 

Amesisitiza kuwa maendeleo ya kweli hayawezi kufikiwa bila ushirikiano wa karibu kati ya viongozi na wananchi, na akawahimiza wakazi wa Songea kuendelea kumuunga mkono kwa mustakabali bora wa jimbo hilo.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...