Na Seif Mangwangi, Arusha
SERIKALI ya Jamhuri ya nchi ya Kenya imeiomba mahakama ya watu na Haki za Binaadam (AfCPHR), kuiongezea muda wa utekelezaji wa hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo kuhusu kulipa fidia jamii ya watu wa Ogiek katika msitu wa Mau nchini humo.
Jamii ya watu wa Ogiek wanaopatikana katika msitu wa Mau nchini Kenya, mwaka 2009 Serikali ya Kenya kupitia mamlaka ya misitu nchini humo iliwaondoa kwa nguvu jamii hiyo kutoka katika msitu huo kwa madai ya kutaka kuuhifadhi jambo ambalo walilipinga na kuamua kufikisha madai yao katika Mahakama hiyo ya Afrika ya Watu na Haki za Binaadam (AfCPHR).
Chini ya shirika la utetezi la Ogiek Peoples Development Program kwa kushirikiana na Kamisheni ya utetezi wa Haki za binaadam Afrika, jamii hiyo ilishinda shauri hilo nambari 006/2012 na Serikali ya Kenya kuamriwa kuwarejeshea jamii hiyo msitu wa Mau ikiwa ni pamoja na kufidia wale wote walioathiriwa na zoezi la kuwaondoa.
Wakiwasilisha maombi hayo mbele ya Mahakama hiyo jana juni4, 2025 waendesha mashtaka kutoka Serikali ya Kenya kutoka ofisi ya wakili Mkuu wa Serikali, Laurence Mwiruri, Charles Mutinda na Christopher Malwa wamesema utekelezaji wa hukumu hiyo iliyotolewa Mei 2017 inachangamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa fedha pamoja na masuala ya kisiasa.
Wamesema pia msitu wa Mau ni sehemu ya eneo ambalo limetengwa kwaajili ya uhifadhi kwa kuwa lina vyanzo vingi vya maji na kwamba Serikali ya Kenya imeingia mikataba ya Kimataifa ya kutunza eneo hilo.
" Waheshimiwa majaji, ningependa kuieleza mahakama hii kwamba Serikali ya Kenya imekubaliana na hukumu iliyotolewa na tumeshaanza utekelezaji wa baadhi ya maagizo ya mahakama ikiwemo kuitambua jamii ya Ogiek kwa kutoa tangazo katika gazeti la Serikali," amesema Naibu wakili Mkuu Christopher Wamalwa mjibu maombi upande wa Serikali ya Kenya.
Wakili Wamalwa amesema katika sensa ya watu na makazi ikiyofanyika mwaka 2019 nchini humo, jamii ya Ogiek pia ilihesabiwa na kupatikana kwa idadi ya 54200 kote nchini Kenya ambapo Katiba ya Kenya imetambua lugha yao.
Amesema pia Serikali ya Kenya kupitia baraza la mawaziri kuliundwa kamati maalum ya kuishauri Serikali namna bora ya utekelezaji wa hukumu iliyotolewa ambapo jopo hilo limeshafanya mazungumzo na jamii ya Ogiek na kufanya mashauriano
Wakili Wamalwa amesema katika mashauriano yaliyofanywa ilibainika kuwa kuna baadhi ya wananchi wameuza maeneo yao kwa watu ambao sio wa jamii hiyo hivyo bado mashauriano yanafanyika ili wale waliouza wasiweze kufaidika zaidi na msitu huo
" Mheshimiwa Jaji, kwa hiyo jopo lililoundwa bado halijamaliza kazi yake, tunaiomba mahakama hii ituongezee muda wa kukamilisha kazi hii na itakapomalizika tutakuja kuieleza mahakama". Walisema mawakili hao.
Upande wa waleta maombi uliokuwa ukiongozwa na Profesa Solomon Dersso wa chuo kikuu cha Pretoria Afrika Kusini na Mkuu wa kamisheni ya Haki za Binaadam aliieleza mahakama kuwa kesi hiyo ni ya muda mrefu lakini serikali ya Kenya imekuwa ikionyesha haiko tayari kufanya utekelezaji wa Hukumu iliyotolewa jambo ambalo ni sawa na kuidharau mahakama hiyo.
Amesema maagizo mbalimbali hayajatekelezwa ikiwemo kupelekwa kwa ripoti ya utekelezaji wa hukutuma hiyo kwa jamii ya Ogiek na kuiomba mahakama hiyo kuiagiza Serikali ya Kenya ni lini haswa itatekeleza hukumu hiyo na wasipotekeleza wachukuliwe hatua gani.
Aidha aliiomba mahakama ipeleke tume ya majaji wastaafu katika msitu wa Mau kuzungumza na wananchi wa jamii hiyo pamoja na kuona namna ambavyo jamii hiyo imekuwa ikiendesha maisha yake
" Serikali ya Kenya inasema imeamua kuchukua msitu wa Mau kwa sababu ya kuutunza, lakini niihakikishie mahakama hii jamii ya Ogiek ni watunzaji wazuri sana wa maliasili, tunaomba warejeshewe msitu wao ili waendeleze maisha pamoja na kutunza maliasili iliyopo ambayo wamekuwa wakiitunza kwa miaka mingi sasa," amesema.
Daniel Kobei mkurugenzi wa tasisi ha utetezi ya Ogiek Community Development Program amesema anaamini jamii ya ogieo itaenda kupata haki yake baada ya Serikali ya Kenya kuanza kutekeleza baadhi ya mambo yaliyoamuliwa kwenye hukumu
Wakili Bahame Nyambuga anayeongoza jopo la mawakili wanaotetea jamii ya Ogiek akiwemo katika wakili Donald Deya wa Pan African Lawyers Union, amesema pamoja na serikali ya Kenya kuendelea kuchelewesha utekelezaji wa hukumu hiyo kwa miaka tisa sasa, bado wataendelea kusubiri.
Majaji katika mahakama hiyo waliutaka upande wa wajibu maombi Serikali ya Kenya kuieleza mahakama hiyo wanataka wapewe muda gani ili kuweza kutekeleza hukumu hiyo kwa kuwa tayari walishapewa muda wa kutosha na bado hawajatekeleza.
Novemba mwaka jana 2024, Serikali ya Kenya iliiomba mahakama hiyo kuwaongezea miezi mitatu ili iweze kutekeleza hukumu hiyo iliyotolewa mwaka 2017 na baadae mwaka 2022 jambo ambalo bado hawajaweza kulitimiza.
Rais wa Mahakama hiyo Jaji Sacko aliahirisha shauri hilo na kusema kuwa maamuzi zaidi kuhusu ombi la serikali ya Kenya juu ya utekelezaji wa hukumu hiyo yatatolewa hivi karibuni.
Serikali ya Kenya imeamriwa mbali ya kuitambua jamii hiyo, lugha wanayoongea na kuwarejesha katika Msitu wa Mau pia imetakiwa kuwakulipa fidia wakazi wa jamii ya Ogiek kiasi cha shilingi Mil158 za Kenya Sawa na Dola Milioni 1.2

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...