Nyasa-Ruvuma.

Katika kuadhimisha na kuelekea kilele Cha wiki ya Mazingira Duniani ambapo kilele ni Tar 05/6 Kila mwaka Taasisi ya Chagei kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Limbo wamefanya usafi wa Fukwe ya ziwa Nyasa Mbamba bay na kutoa vifadhia taka Ili kulinda na kutunza mazingira hayo kwa Vizazi Endelevu.

Zoezi Hilo limefanyika kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo,wavuvi wa eneo Hilo,wanafunzi na Wananchi wa eneo Hilo.

Akizungumza Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Furaha Wanjarwa ameipongeza Taasisi hiyo kwa kuendesha zoezi Hilo na wao kama Halmashauri watakuwa wakifanya mara kwa mara huku akiwataka Wananchi na wavuvi wanaofanya shughuli zao kuzunguka maeneo ya Fukwe za ziwa Hilo kufanya usafi wa mara kwa mara.

Naye Afisa mazingira Wilaya hiyo Denis William amesema wadau mbalimbali na Wananchi wawe na kawaida ya kufanya usafi katika mazingira yao na sio TU katika Fukwe za bahari na wao Viongozi wapo tayari kutoa ushirikiano wakati wowote

Aidha Mwenyekiti wa Wavuvi (BMU) Adrea Ligola amesema ujio wa Chagei umewatia moyo na wao Kila jumamosi ya mwisho wa mwezi huwa wanafanya usafi na wejifunza kuwa na ushirikiano.

Naye Mwalimu wa walezi wa wananfunzi marafiki wa Chagei katika shule ya Sekondari Limbo Beatrice Milinga amesema wao watakuwa mabalozi wazuri wa chagei Nyasa na wanaenda kufungua Club ya Chagei katika shule hiyo kwa lengo la kuhamasisha utunzaji wa mazingira na upandaji wa miti

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Chagei David Haule ameeleza wao jukumu lao kubwa ni kutunza usafi wa mazingira na kushughulikia masuala ya kijinsia na kufanya usafi ziwa Nyasa ni moja ya mpango kazi wao kama Taasisi na itakuwa Endelevu huku, akitoa pongeze na shukran kwa ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kwa kutoa ushirikiano mkubwa na jambo hili watakuwa wakifanya Kila mwaka.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...