Dodoma, Tanzania, Juni 10, 2025 - Wizara ya Kilimo na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japani (JICA) leo wamekutana katika mkutano wa pili wa Kamati ya Pamoja ya Uratibu (JCC) cha Mradi wa Kuimarisha uwezo wa Wadaui wa Sekta ya Mpunga Tanzania (TANRICE3) katika Hoteli ya Rafiki mjini Dodoma. Mkutano huu umewakutanisha wadau hao ili kutathmini maendeleo na kupanga mwelekeo wa baadaye wa ukuzaji wa sekta ya mchele nchini Tanzania.
TANRICE3, ilizinduliwa mwezi Juni 2023, inalenga kuongeza uzalishaji wa mchele nchini Tanzania kupitia mipango kabambe wa kujenga uwezo unaolenga wakulima, maafisa ugani, na taasisi za kilimo. Mradi huu umetokana na mashirikiano ya zaidi ya miaka 40 ya kilimo kati ya Japan na Tanzania, ambao ni mwendelezo wa programu za awali za TANRICE na TANRICE2 ambazo zimechangia kwa kiwango kikubwa katika kuleta mabadiliko ya sekta ya mchele nchini.
Kwa mwaka uliopita, mradi huu umepata matokeo mazuri ambapo zaidi ya 2,384 katika maeneo 27 tofauti walifundishwa mbinu za kilimo cha mpunga cha umwagiliaji. Uzalishaji wa mpunga katika maeneo yanayotegemea kilimo cha umwagiliaji umeongezeka kutoka tani 3.25/ha hadi tani 4.63/ha, sawa na ongezeko la 40% ya mavuno. Mradi huu pia umeanzisha mfumo wa kijiditali wa mkakati wa maendeleo ya mapunga Nchi (NaRDA), ili kuweza kusimamia na kutunza taarifa za mafunzo yanayofanyika ili kusaidia .
"Mradi huu ni moja wa miradi unawakilisha mashirikiano yaa zaidi ya miaka 40 kati ya Japan na Tanzania katika sekta ya kilimo," alisema Bwana Seizaburo Asano, Mwakilishi wa JICA Tanzania. "Maono yetu yanapanuka zaidi ya mradi ambapo sekta ya mpunga ya Tanzania inakua kwa kujitegemea, ikiungwa mkono na taasisi imara za za ndani na wafanyakazi waliofunzwa vizuri."
Katika hotuba yake ya ufunguzi, Dk. Wilhelm Mafuru, Mkurugenzi wa Mafunzo na tafiti, Wizara ya Kilimo, alitoa JICA kwa kutoa msaada wa maendeleo tangu miaka ya 1970, akisisitiza kwamba mpunga unabaki kuwa zao muhimu la kimkakati kwa nchi. Alithibitisha dhamira thabiti ya wizara katika kuhakikisha uendelevu wa shughuli na matokeo ya TANRICE3.
Mradi huu unaendana na Mkakati wa Maendeleo ya sekta ya Mpunga Tanzania (NRDS-II) na unachangia lengo la nchi la kufikia uhakika wa mchele huku ukichangia katika usalama wa chakula katika kanda. TANRICE3 ni mfano wa ushirikiano wa kudumu kati ya Japani na Tanzania katika uendelezaji wa kilimo na ubora na ustawi wa maisha ya vijijini.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...