Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Dkt Pindi Chana amesema kuwa Tanzania imepewa heshima ya kuwa mwenyeji katika tukio la utoaji Tuzo za Utalii Duniani Kanda ya Afrika na Bahari ya Hindi kwa mwaka 2025 zinazofahamika kama World Travel Award.
Mhe Chana amesema hayo mapema Leo hii Jijini Dodoma Juni 26,2025 wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu utoaji wa Tuzo hizo ambazo zinatarajiwa kufanyika Jijini Dar es Salaam Juni 28,2025.
Na kusema kuwa Tanzania kuwa Mwenyeji katika tukio hili ni uthibitisho wa hadhi ambayo Nchi imejipatia Kimataifa katika Sekta ya Utalii na matokeo ya kazi kubwa inayofanywa na Rais wa awamu ya sita Dkt Samia Suluhu Hassan.
"Kwa furaha kubwa, ninapenda kutumia fursa hii kuwajulisha kuwa Tanzania imepewa heshima ya kuwa mwenyeji wa tukio la utoaji Tuzo za Utalii Duniani Kanda ya Afrika na Bahari ya Hindi kwa mwaka 2025 (World Travel Awards), hafla ya tukio hilo itafanyika siku ya Jumamosi, tarehe 28 Juni, 2025,Jijini Dar es Salaam".
"Ndugu WanahabariTanzania kuwa mwenyeji wa tukio hili la kimataifa ni uthibitisho wa hadhi kubwa ambayo nchi yetu imejipatia kimataifa katika Sekta ya utalii. Aidha, ni matokeo ya kazi kubwa inayofanywa na Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa kinara wa kutangaza Utalii kupitia filamu ya Tanzania, the Royal Tour na Amazing Tanzania pamoja na jitihada zingine zinazofanyika katika kuendeleza na kukuza utalii nchini".
Aidha amesema Tuzo hizi za World Travel Award zilianzishwa mwaka 1993 nchini Uingereza chini ya Kampuni ya World Luxury Media Group ambapo zimefanyika kwa miaka 32 mfulululizo zikiwa na lengo la kutambua na kutoa hadhi kwa watoa huduma za utalii.
Na pia Tuzo kuendelea kujipatia umaarufu na kuwa Jukwaa rasmi la kutangaza utalii kwa nchi zinazoshiriki ambapo na sisi Tanzania tulianza kushiriki mwaka 2013 ambapo tulishinda Tuzo ya Kivutio Bora Barani Afrika ambacho ni Mlima Kilimanjaro na tuliendelea kushiriki hadi kufikia mwaka 2024 ambapo tulifanikiwa kushinda Tuzo tano.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...