Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) imeeleza kuwa katika kipindi cha miaka 50 tangu kuanzishwa kwake, imefanikiwa kufanya tafiti mbalimbali zilizosaidia kuimarisha uwezo wa kufanya maamuzi ya kisera kuhusu masuala ya ufundishaji na ujifunzaji, kwa kutumia ushahidi wa kitaalamu unaotokana na matokeo ya tafiti hizo.
Akizungumza leo Juni 13, 2025 jijini Dar es Salaam katika semina ya wahariri na waandishi wa habari kuelekea maadhimisho ya miaka 50 ya TET, Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo, Dkt. Aneth Komba, amesema tafiti hizo zimekuwa zikiendeshwa kwa kushirikiana na vyuo vikuu mbalimbali vya ndani na nje ya nchi, hatua ambayo pia imeimarisha mapato ya ndani ya taasisi.

Tafiti Zenye Mchango Mkubwa kwa Elimu
Dkt. Komba ametaja baadhi ya tafiti zilizofanywa na TET, ikiwemo ile ya mwaka wa fedha 2020/2021 iliyoshirikisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Aga Khan, Aga Khan Foundation (AKF) na EdTech Hub. Utafiti huo ulilenga kubainisha teknolojia nafuu, sahihi na endelevu ya TEHAMA inayofaa kwa mafunzo ya walimu waliopo kazini, hasa maeneo ya vijijini, kwa lengo la kuboresha matokeo ya wanafunzi wa shule za msingi.
“Tafiti hii ilitumia Shilingi milioni 850, na matokeo yake yameanza kusaidia kutoa ushauri juu ya teknolojia zinazofaa zaidi kwa mazingira ya vijijini, Utafiti huu ulitumia kiasi cha Sh. Milioni 850, tumepata matokeo ya utafiti huu na tunatarajia kuwa yatatusaidia kushauri teknolojia ambayo ni nafuu na inaweza kutumika katika mazingira ya vijijini,” amesema
Hata hivyo amesema kwa mwaka wa fedha 2021/2022 TET imefanya utafiti na Chuo Kikuu cha Western Norway of Applied Sciences ambao unaojulikana kama ‘Kuona ni Kujifunza’ ambao lengo lake lilikuwa ni kubaini changamoto za uoni miongoni mwa wanafunzi wa elimu ya awali na msingi na kutoa afua stahiki.
Amesema matokeo ya utafiti huo yamepelekea uhitaji wa kuandaa moduli kwa kutolea mafunzo kazini kwa walimu ili kuongeza umahiri wao katika kuwabaini, kuwachunguza na kutoa afua stahiki kwa wanafunzi wenye changamoto za uoni katika kujifunza kuanzia elimu ya awali hadi sekondari na kwamba jumla ya fedha iliyotumika katika utafiti huu ni Sh. Milioni 950.

Utafiti wa Kimataifa Wenye Uwekezaji Mkubwa
Kwa mwaka wa fedha 2023/2024, TET inatekeleza utafiti wa miaka mitano ujulikanao kama “What Works Hub (WWH) for Global Education”, kwa kushirikiana na Vyuo Vikuu vya Georgetown, Delaware na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam - Ndaki ya Elimu. Kupitia utafiti huu, kituo cha utafiti kiitwacho TIE-Ed-Lab kimeanzishwa, kikilenga kufanya tafiti bunifu katika ufundishaji na ujifunzaji ili kusaidia maamuzi ya kielimu yanayozingatia ushahidi.
“Kupitia utafiti huu kituo cha utafiti kiitwacho “TIE-Ed-Lab kimeanzisha. Kituo hiki kimejikita kufanya tafiti mbalimbali katika masuala ya ufundishaji na ujifunzaji kwa ujumla ili kuendelea kuimarisha utoaji wa maamuzi unaotumia na matokeo ya tafiti,” amesema
Amesema utafiti huo ni wa miaka mitano na utagharimu zaidi ya Sh. Bilioni 7 na kuongeza kuwa katika miaka hiyo 50 wamefanikiwa kuongezeka kwa ushirikiano wa TET na taasisi nyingine za ndani na nje katika kutekeleza majukumu ya taasisi.
Ushirikiano Mpana na Taasisi za Ndani na Nje
Kwa mujibu wa Dkt. Komba, kufikia mwaka 2025, TET imeingia mikataba ya ushirikiano na taasisi na mashirika 35, yakiwemo yanayojihusisha na matumizi ya akili mnemba (Artificial Intelligence – AI) katika ufundishaji, pamoja na uandaaji wa maudhui ya kidijitali kwa ajili ya viwango mbalimbali vya elimu.
Kwa mujibu wa TET, mafanikio haya yanadhihirisha nafasi muhimu ya tafiti katika kuimarisha sekta ya elimu nchini, hususan kwa kuleta ushahidi wa kisayansi unaosaidia kufanya maamuzi sahihi, kutatua changamoto za ujifunzaji na kuendeleza ubunifu wa kiteknolojia unaolenga mazingira halisi ya shule za Tanzania.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...