Na Janeth Raphael MichuziTv

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Profesa Elisante Ole Gabriel amekabidhiwa Makombe kumi na tano (15) pamoja na Medali toka kwa timu ya Mahakama hiyo huku wakiomba kuongezewa muda wa kufanya mazoezi ili waweze kutwaa ubingwa wa jumla katika michuano ijayo ya Mei Mosi na ile ya SHIMIWI.

Akizungumza wakati akikabidhi makombe hayo,Katibu wa timu ya michezo ya Mahakama, Robert Tende alisema timu hiyo imeshika nafasi ya nne katika michuano ya Mei Mosi iliofanyika Mei mkoani Singida na hiyo imetokana na ufinyu wa muda wa kufanya mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na michuano mbalimbali wanayoshiriki.

Tende amesema kikosi cha michezo mbalimbali cha timu hiyo,kama riadha,netiboli,soka,timu ya kuendesha baiskeli, darts pamoja na Karata wanahitaji muda zaidi wa kufanya mazoezi ili waweze Kuga ya vizuri katika michuano ijayo.

"Tunaomba tuongezewe muda wa kujiandaa na mashindano mbalimbali tunaweza kufanya vizuri zaidi ya mwaka huu katika michiluano ya Mei Mosi na SHIMIWI,"alisema Tende.

Aidha amesema lengo lao ni kuona kila mwaka timu hiyo inafanya vizuri.na kurejea na makombe katika michuano mbalimbali,"alisema Tende.

Naye mgeni rasmi katika hafla hiyo,Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania,Profesa Elisante Ole Gabriel amesema ombi la lao la kuongezewa muda wa mazoezi litafanyiwa kazi Kwa sababu michezo nayo ni sehemu ya kazi.

Prof Ole Gabriel amesema timu ya Mahakama ikifanya vizuri inakuwa imeitangaza mahakama katika maeneo mbalimbali ukiacha kazi nzuri ya kutoa haki wanayofanya hata kwenye michezo wanashiriki na kufanya vizuri.

"Nitazingatia maombi yenu na kuyafanyia kazi kwa sababu ili la muda wa mazoezi lipo ndani ya uwezo wangu hivyo nitalifanyia kazi ili timu yeti iweze kusonga mbele,"alisema Prof Ole Gabriel.

Mbali na hilo aliipongeza timu hiyo kutokana na kufanya vizuri katika michezo mbalimbali pamoja na kuwakabidhi vyeti washindi vya kuonyesha mahakama inatambua mchango unaofanywa na timu ya michezo ya Mahakama ya Tanzania.

Hata hivyo Profesa Elisante amesema Mahakama inajipanga kuomba mechi ya kirafiki dhidi ya Simba na Yanga na timu nyingine zinazoshiriki ligi kuu iki waweze kujipima nguvu.

Amesema anatamani kuiona timu ya michezo ya mahakama inacheza mechi kubwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa pamoja na timu zinazoshiriki ligi Kuu ya Bara.

Aidha ametoa rai kwa viongozi wa timu hiyo kuita wachezaji kutoka mikoa mbalinbali ili mradi ni watumishi wa mahakama ya Tanzania ili waweze kuungana na timu hiyo kuongeza nguvu kwenye kikosi cha timu hiyo.

Mwajabu Bwire ambaye ni mshindi wa mashindano ya Baiskeli alisema,michuano ya Mei Mosi ilikuwa na ushindani mkubwa lakini alijitahidi kuhakikisha anaipa ushindi timu ya michezo ya Mahakama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...