Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, leo Juni 12, 2025 amewasilisha Hotuba ya hali ya uchumi nchini kwa mwaka 2024 na mpango wa maendeleo wa taifa wa mwaka 2025/26, Bungeni jijini Dodoma.
Akiwasilisha hotuba kuhusu Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2025/26, Prof. Mkumbo amesisitiza kuwa Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi, itajikita katika kuendeleza miradi ya kielelezo yenye manufaa na matokeo makubwa ili kutimiza vipaumbele vitano vikuu.
Vipaumbele hivyo ni pamoja na:
• Kuchochea uchumi shindani na shirikishi.
• Kuimarisha uwezo wa uzalishaji wa bidhaa viwandani na utoaji huduma.
• Kukuza uwekezaji na biashara.
• Kuchochea maendeleo ya watu.
• Kuendeleza rasilimali watu.
Hali ya Uchumi kwa mwaka 2024: Pato halisi la Taifa (GDP) lilifikia Shilingi trilioni 156.6 mwaka 2024, ikilinganishwa na Shilingi trilioni 148.5 mwaka 2023. Hii inawakilisha ukuaji wa asilimia 5.5, ikiongezeka kutoka asilimia 5.1 mwaka uliopita.
Ukuaji huu unatokana na sababu mbalimbali, ikiwemo:
• Kuanza kwa uzalishaji wa umeme katika Bwawa la Julius Nyerere.
• Utekelezaji endelevu wa miradi ya kimkakati ya miundombinu.
• Usimamizi thabiti wa sera za fedha.
• Kuimarika kwa uzalishaji wa mazao ya kilimo.
• Uwekezaji wa Serikali katika huduma za jamii kama elimu, afya, maji, na hifadhi ya jamii.
Sekta tano zilizochangia zaidi ukuaji mwaka 2024 ni pamoja na:
• Sanaa na burudani (17.1%)
• Uzalishaji na usambazaji wa umeme (14.4%)
• Habari na mawasiliano (14.3%)
• Fedha na bima (9% na 13.8% mtawalia)
• Afya (10.1%).
Mpango uliyowasilishwa leo ni kiungo kati ya mipango inayokamilika na mipango mipya inayotarajiwa kutekelezwa chini ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, kwa mujibu wa Mhe. Waziri utajielekeza katika kuainisha na kutekeleza programu na miradi muhimu ambayo haijakamilika ili kuandaa mazingira shirikishi na endelevu kwa mipango ijayo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...