Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma

Imeelezwa kwamba vituo saba vya Tanzania Bara vimefanikiwa kuendesha mitihani ya BODI ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) ambapo jumla ya watahiniwa 1,506 walisajiliwa na 1,421 waliratibiwa kufanya mitihani.

Taarifa hiyo imetolewa Jijini Dodoma leo na Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB Godfred Mbanyi ambaye amesema kwa ujumla watahiniwa walifaulu mitihani yao, huku 610 wakitakiwa kurudia baadhi ya masomo na 131 wamefeli mitihani yote.

Amebainisha, “Masomo yaliyofanywa vizuri zaidi ni Michakato ya Zabuni na Majadiliano ya Kimkataba, ambapo watahiniwa walionyesha uelewa mzuri na matokeo chanya,”

Aidha Bodi imeainisha masomo yanayohusisha hesabu yameendelea kuwa changamoto kubwa kwa watahiniwa wengi, hivyo ipo haja ya kuwepo kwa maandalizi mazuri zaidi ili kufikia viwango vinavyokusudiwa.

Katika hatua nyingine, uongozi wa Bodi umewapongeza watahiniwa waliopata mafanikio na kuwataka wahadhiri kufuata maelekezo ya Bodi katika kutoa mafunzo ili kuhakikisha Nchi inazalisha wataalamu bora wenye mchango katika maendeleo ya Taifa.

Huku mkazo ukiwekwa kwa watahiniwa waliopata changamoto katika mitihani hiyo kujiandaa vyema kwa ajili ya mitihani ya marudio itakayofanyika mwezi Novemba mwaka huu, huku wazazi na walezi wakihimizwa kuendelea kuwapa moyo vijana wao.

Ameongeza kusema, "Moja ya changamoto iliyojitokeza katika mtihani huo ni baadhi ya watahiniwa kujihusisha na vitendo vya udanganyifu kutokana na maandalizi duni, hali iliyotajwa kuwa kinyume na maadili ya taaluma hiyo inayohitaji uadilifu wa hali ya juu,”


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...