Watanzania maarufu na wasio maarufu waliungana jijini Dar es Salaam Jumanne kusisitiza faida muhimu za mazingira na umuhimu wa juhudi za pamoja za uhifadhi.
Tukio hilo lilisisitiza kwamba bila kujali sisi ni nani au tunatoka wapi, sote tunahusiana na mazingira na ni wajibu wetu kuyatunza.

Mwimbaji na mtangazaji wa Televisheni Nakaaya Sumari, waimbaji wawili maarufu Navy Kenzo,na Kiongozi mpya wa Shirika la Afya Duniani kanda ya Afrika, kutokea Tanzania, Profesa MohamedJanabi, wote wanatoa sauti zao kuunga mkono mazingira.

Kuungwa mkono na watanzania wenye asili mbalimbali, kunatukumbusha juu ya uhusiano wa kina wa kitaifa na kibinafsi ambao sotetunao juu ya mazingira na huduma zake nyingi nzuri - kuanzia uzuri na hamasa, hadi kwenye ajirana afya.
Akizungumza wanahabari na wadau mbalimbali katika studio za TBC, Sumari alibainisha kuwa mazingira ni Tanzania, na mazingira hayo ni kwa kila mtu. Alihimiza kila mtu kutumia siku nzima kwenyemazingira ya asili na familia zao au marafiki, wakiyathamini na kutafakari juu ya maana yake kwao.

Namna nyingine za kuwa mhifadhi zilizopendekezwa na Nakaaya ni kutokula nyama ya mwituisiyodhibitiwa, kutotupa taka za plastiki mahali ambapo haparuhusiwi, au kufikiria mara mbilikabla ya kukata mimea au miti.

Hassan Sengo, dereva wa boda boda ambae nae ni mwanafamilia wa Nihifadhi alisimama kuwaanafaidika na mazingira ya kila siku, kwani kijiwe chake cha boda boda kipo chini ya mtiwa mwarobaini ambao hutoa kivuli.
Hassan alisisitiza kuwa haijalishi taaluma ya mtu, iwe anaishi kijijini au mjini, mazinigira hutupatia kitu kizuri na mazingira rafiki wakati wa utendaji wa kazi zetu sisi sote.

Pia katika kuhamasisha kwa jamii kuhakikisha kila mtanzania anakuwa muhifadhi kuna video mpya kuna wasanii wawili maarufu Navy Kenzo. "Tunapata ubunifu wanyimbo zetu kutoka kwenye mazingira," waimbaji walisema.

“Ni muhimu, na kama Watanzania,utambulisho wetu wa kitamaduni, maendeleo ya kitaifa, na matarajio ya baadaye yategemee sanakutumia mazingira kwa uendelevu, na kwa maana hiyo ni lazima sote tuwe wahifadhi. Sisi ni wahifadhi!”Tanzania na mazingira vimeunganishwa kwa namna ya ndani na ya msingi ambayo haiwezi kutenganishwa.

Asili na utamaduni wetu mwingi unatokana na mazingira ya asili, na tuna historiandefu ya kuishi pamoja kwa uendelevu na mazingira. Mazingira hutoa rasilimali katika mtindo wamaisha yetu na mandhari yetu ya ajabu, na hutoa udongo wetu wenye rutuba na bahari safi.

Tanzania ni nyumbani kwa idadi kubwa ya simba ulimwenguni na ya pili kwa idadi kubwa yatembo, na tunapata karibu 18% ya pato letu la Taifa na ajira milioni 1.5 kila mwaka kutokana nautalii, ambao unaendeshwa sana na utalii.

Katika maeneo ya vijijini, mapato yanayotokana na utalii hutiririka moja kwa moja kwenda kwenye jamii kugharamia shule, vituo vya afya na miundombinu.




 Ujumbe mkubwa ni: ikiwa wewe ni Mtanzania, una uhusiano na mazingira, unaweza kuchukuajukumu lako mwenyewe katika kuyalinda.

Kampeni ya Mimi ni Muhifadhi inalenga kukuza hisia ya uwajibikaji wa pamoja, na kuwahamasisha Watanzania wote kujitambulisha kama wahifadhi. Niukumbusho kwamba kuhifadhi mazingira yetu kunanufaisha maisha yetu ya kila siku na ustawi,pamoja na yale ya vizazi vijavyo.

Katika mgahawa wa kahawa jijini Dar es Salaam, mhudumu Neema Mduma aliulizwa mazingira yana maana gani kwake. "Furaha," alijibu.Kampeni hii inaungwa mkono na Community Wildlife Management Areas Consortium (CWMAC),Honeyguide Foundation na WildAid na inadhaminiwa na Shirika la Utangazaji la Tanzania na SafariChannel.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...