Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya waratibu, waandishi wasaidizi na waendesha vifaa vya bayometriki wa Magereza kuhusu uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura yaliyoanza leo Juni 22 -24, 2025 mkoani Dodoma.

Sehemu ya washiriki wa mafunzo ya siku tatu ya Waratibu, Waandishi Wasaidizi na Waendesha vifaa vya Bayometriki wa Magereza kuhusu uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura yaliyoanza leo Juni 22 -24, 2025 mkoani Dodoma.

Hakimu Denis John Mpelembwa akiwaapisha washiriki
Washiriki wa mafunzo ya siku tatu ya Waratibu, Waandishi Wasaidizi na Waendesha vifaa vya Bayometriki wa Magereza kuhusu uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura yaliyoanza leo Juni 22 -24, 2025 mkoani Dodoma wakila kiapo cha kutunza siri kabla ya kuanza mafunzo hayo.Mratibu wa Uandikishaji ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mafunzo , akizungumza jambo.
Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji, Caroline Ruben akiwasilisha mada kuhusu uraia kwa washiriki wa mafunzo hayo.
******
Na. Waandishi Wetu
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imewaasa watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwenye Magereza kwa Tanzania Bara na Vyuo vya Mafunzo kwa Tanzania Zanzibar kufanya kazi kwa weledi.
Wito huo umetolewa wakati wa ufunguzi wa
mafunzo ya siku tatu kwa watendaji hao ambayo yameanza leo tarehe 22 Juni, 2025
Mkoani Dodoma kwa Magereza sambamba na Unguja kwa Vyuo vya Mafunzo.
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imewaasa watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwenye Magereza kwa Tanzania Bara na Vyuo vya Mafunzo kwa Tanzania Zanzibar kufanya kazi kwa weledi.
Akifungua
mafunzo kwa watendaji hao yaliyofanyika Mkoani Dodoma kwa watendaji wa
Magereza, Tanzania Bara, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa
Mahakama ya Rufani, Mhe. Jacobs Mwambegele amesema Tume imewateua watendaji hao
kutokana na weledi wao.
“Sina shaka kuwa kuteuliwa kwenu kunatokana
na ujuzi, uwezo na weledi mlionao katika kutekeleza majukumu ya kitaifa
likiwepo zoezi la uboreshaji wa Daftari ambalo ni sehemu ya maandalizi ya
Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025,” amesema Mhe. Mwambegele.
Amewahakikishia watendaji hao kuwa kwenye
mafunzo hayo ya siku tatu Tume itawapa ujuzi wa kutosha kwa nadharia na vitendo
kuwawezesha kutekeleza jukumu lao kwa weledi.
Akifungua mafunzo kama hayo Kisiwani Unguja,
Zanzibar kwa watendaji wa Vyuo vya Mafunzo, Makamu Mwenyekiti wa Tume, Jaji wa
Rufani Mstaafu, Mhe. Mbarouk Salim Mbarouk ametoa wito kwa watendaji hao kuvitunza
vifaa vya uboreshaji wa daftari.
“Ninatoa wito kwenu kuhakikisha mnavitunza
vifaa vyote vitakavyotumika katika zoezi la uboreshaji wa Daftari na kuzingatia
maelekezo yote yatakayotolewa na Tume ili muweze kuyafanyia kazi kwa usahihi
wakati wote wa utekelezaji wa zoezi hilo,” amesema.
Jaji Mbarouk pia amewahakikishia watedaji hao
kuwa maafisa kutoka Tume watakuwepo muda wote wa zoezi na kwamba endapo
watapata changamoto ya aina yoyote wasisite kuwasiliana nao.
Kwa mujibu wa ratiba zoezi hilo la uboreshaji
wa Dafatri kwenye Magereza na Vyuo vya Mafunzo linafanyika kwa siku saba
kuanzia tarehe 28 Juni hadi tarehe 04 Julai, 2025 ambapo watakaohusika ni
mahabusu na wafungwa walihukumiwa kifungo chini ya miezi sita.Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe, Jaji wa Rufani (Mstaafu), Mbarouk Salim Mbarouk akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya waratibu, waandishi wasaidizi na waendesha vifaa vya bayometriki wa Vyuo vya Mafunzo kuhusu uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura yaliyoanza leo Juni 22 -24, 2025 Mjini Unguja Zanibar.
Mkurugenzi wa Ofisi ya Zanzibar, Ndg. Adam Mkina akizungumza wakati wa Mafunzo hayo.
Mkurugenzi wa Ofisi ya Zanzibar, Ndg. Adam Mkina akizungumza wakati wa Mafunzo hayo.
Meza Kuu ikiwa katika mafunzo hayo.
Mafunzo yakiendelea
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...