Na Seif Mangwangi, Arusha

WIKI ya Asasi za kiraia 2025 (AZAKI) inaanza kesho jumatatu Juni2 hadi 6, 2025 Jijini Arusha huku washiriki zaidi ya 900 kutoka taasisi mbalimbali nchini ikiwemo mashirika na taasisi binafsi wakitarajiwa kushiriki.

Akizungumza kwenye kikao na waandishi wa habari leo Juni1, 2025 jijini Arusha, Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for civil society(FCS), Justice Rutenge amesema Waziri wa nchi ofisi ya Rais Mipango na uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo atakuwa mmoja wa wazungumzaji katika wiki ya AZAKI mwaka huu.

Rutenge amesema katika msimu huu wa maadhimisho ya wiki ya asasi za kiraia mjadala mkubwa utajikita kwenye tathmini ya asasi za kiraia nchini pamoja na dira ya Taifa ya Maendeleo 2025-2050.

Ameishukuru serikali kwa kushirikisha kikamilifu asasi za kiraia katika utoaji wa mawazo katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 na kuhakikisha sekta ya elimu nchini inakuwa ni moja ya sekta za kimapinduzi, ili kusaidia utekelezaji wa dira uendane na wakati ikiwemo matumizi ya Tehama.

Rutenge amesema ushirishwaji wa azaki katika utoaji mchango wa Dira ya Taifa 2050 ni mkubwa na wametoa mapendekezo yao zaidi katika suala zima la elimu hususan katika matumizi ya teknolojia ya Tehama ili kuwezesha wanafunzi kuhakikisha wanapambana na kasi ya teknolojia inayokua kwa kasi Duniani.

"Kwa mara ya kwanza Serikali imeshirikisha vyema asasi za kiraia aidha kwa mtu mmoja mmoja au taasisi katika uundwaji wa dira ya Taifa na kukuza uchumi endelevu na sisi tumesema sekta ya elimu ni muhimu katika kuhakikisha inakua ikiwemo kwenda na kasi ya Tehama inayokuwa zaidi Duniani,"amesema

Mwenyekiti wa Bodi ya Foundation for Civil Society(FCS), CPAT Mercy Silla amesema FCS inajivunia mambo mengi ikiwemo kufanya maadhimisho ya wiki ya AZAKI kwa miaka saba mfululizo huku lengo kuu likiwa ni kuwaleta pamoja wadau wa sekta ya Azaki na kufanya mijadala mbalimbali ya maendeleo kwa mustakabali wa nchi.

"Kila mwaka tuna utaratibu wa kuangazia mambo mbalimbali na kuweka sawa Maudhui ya wiki ya Azaki na mwaka huu tutaangazia mchakato mzima wa dira ya Taifa na tunajivunia maendeleo kwani ni wakati sasa wakuangalia jinsi ya kujiendesha mashirika haya wenyewe pasipo kutegemea wahisani lazima tuweke mbinu za kujikwamua wenyewe,"amesema

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya wiki ya AZAKI ambaye pia ni Mkurugenzi mkaz wa asasi ya CBM International, Nesia Mahenge amesema wiki hiyo mwaka huu pia inalenga kutatua changamoto ambazo zipo katika azaki za kiraia na kuona ni namna gani zinatatuliwa.

Amesema mashirika binafsi kama vodacom, Benki za NMB na Stanbic yameshirikishwa katika maadhimisho hayo ambapo mbali ya kuchangia sehemu ya fedha kwaajili ya kufanikisha wiki hiyo pia yatawezesha jamii kwa kutoa elimu mbalimbali ya masuala ya fedha na uwekezaji.

Naye Katibu Mkuu wa Baraza la Mashirika yasiyo ya kiserikali (Nacongo), Adamson Nsimba amesema katika wiki hiyo wataangalia jinsi ya kupanga mikakati ya kuendesha shughuli zao bila kutegemea zaidi msaada ili wasipate mkwamo.

"Tunasema hili sababu tunapata changamoto kila panapotokea mabadiliko ya kidunia ya kisiasa yanatuathiri sana, kama nchini Marekani ilipotokea akaingia Rais Donald Trump amezuia misaada mingi ambayo ndio tegemeo kwa taasisi zetu nyingi na kusababisha kuyumba na baadhi kusimamisha shughuli zao, tunaenda kuangazia namna ya kuweza kujitegemea"
Mkurugenzi wa Foundation for civil society, Justine Rutenge akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), leo 1 Juni 2025

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...