Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde amezindua rasmi kituo cha Polisi Ngwala chenye hadhi ya daraja la C kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi wa kata hiyo pamoja na viunga vyake, kituo hicho kimejengwa na kampuni ya Madini ya Mamba kilichopo kata ya Ngwala Wilaya na Mkoa wa Songwe.
Akizindua kituo hicho Juni 04, 2025 Mh. Mavunde ameeleza dhumuni la kujenga kituo hicho kuwa ni kusogeza huduma za Kipolisi jirani na wananchi kutokana na muingiliano wa watu na mzunguko wa fedha kuwa mkubwa katika eneo hilo kutokana na shughuli za uchimbaji wa madini adimu duniani.
"Uwepo wa kituo hiki ni pamoja na kusaidia kupunguza uhalifu ili shughuli za kiuchumi ziendelee kwa amani na kuweza kuwanufaisha wananchi wa Kata hii na maeneo jirani" alisema Mhe Mavunde.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Augustino Senga ameishukuru kampuni hiyo kwa kujenga kituo hicho pia amewasilisha salamu za pongezi kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania lGP Camillus Wambura kwa kumpongeza Mh. Waziri wa Madini kwa kuzindua kituo hicho pamoja na kuwashukuru wananchi wa Kata hiyo na kuwaomba ushirikiano kuendelea kuwa karibu na Jeshi la Polisi ili kata hiyo kuendelea kuwa salama.
"Jukumu letu kwa sasa ni kuleta Askari kwenye kituo hiki, wananchi mnakaribishwa kutoa malalamiko yenu lakini pia nawaomba msiwe mbali na Polisi kwani kazi za Polisi si zetu peke yetu tunawategemea katika kukilinda kituo hiki ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa za wahalifu ili ziweze kushughulikiwa kwa haraka kwa lengo la kutimiza ujengwaji wa kituo hiki" alisema Kamanda Senga.
Naye, Mtendaji Mkuu wa Mgodi huo Ismail Diwani alisema kuwa lengo la kujenga kituo hicho ni kuendeleza ushirikiano na taasisi za Serikali kwa ajili ya kufikisha huduma kwa jamii hasa katika masuala ya elimu, afya na usalama ili jamii iendelee kuwa salama katika maendeleo ya uchumi wa taifa.
Ikumbukwe kuwa Kituo cha Polisi Ngwala kilitarajiwa kuzinduliwa Aprili 28, 2025 ila ilishindikana kutokana na sababu mbalimbali za kazi za kitaifa za Mh. Waziri Mavunde. Kituo hicho kinalenga kuwa muarobaini wa kutanzua changamoto za kata hiyo za kiusalama na uhalifu wa aina zote.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...