Farida Mangube, Morogoro
Wizara ya Fedha imetoa wito kwa taasisi za umma kuhakikisha fedha za serikali zinasimamiwa ipasavyo ili ziweze kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi.
Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo katika warsha ya siku moja ya kuwajengea uwezo juu ya Mnyororo wa ugavi wahariri wa vyombo vya habari, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Jenifa Christian Olomo amesema Serikali imekuwa ikipoteza fedha nyingi kutokana na ukosefu wa usimamizi mzuri katika ununuzi na usambazaji wa bidhaa na huduma.
“Lazima tuhakikishe kuwa bidhaa au huduma zinazotolewa kwa wananchi ni bora, na fedha zilizotumika zinaendana na thamani halisi. Hii ndiyo njia pekee ya kuhakikisha maendeleo tunayoyazungumzia yanamfikia mwananchi wa kawaida,” amesema Omolo.
Warsha hiyo imelenga kuwajengea uwezo wahariri wa vyombo vya habari ili waweze kuelewa kwa undani nafasi ya minyororo ya ugavi katika maendeleo ya taifa, kuanzia hatua ya kupanga manunuzi, ununuzi, usambazaji hadi huduma kufika kwa walengwa.
Omolo ameeleza kuwa vyombo vya habari vina nafasi kubwa katika kusaidia wananchi kuelewa mchakato mzima wa matumizi ya fedha za umma.
“Wahariri ni watu muhimu kwa sababu wanatoa mwelekeo wa taarifa. Tunawahitaji kusaidia kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa uwazi, uwajibikaji na matumizi sahihi ya fedha za maendeleo,” aliongeza.
Kamishna wa Idara ya Sera za Umma kutoka Wizara ya Fedha, Dk Frederick mwakibinga, amesema sheria ya ununuzi wa umma ni sehemu ndogo ya mfumo mpana wa minyororo ya ugavi, ambao huanzia kwenye upangaji wa mahitaji hadi bidhaa au huduma kufika kwa mlaji wa mwisho ambaye ni mwananchi wa kawaida.
“Tunapozungumzia manunuzi ya serikali, hatumaanishi tu ununuzi wa bidhaa, bali pia kuhakikisha kuwa bidhaa hizo zinafika kwa wakati, kwa ubora na kwa idadi inayohitajika,” alisema Dkt. Mwakipanga.
Alifafanua kuwa hatua zote za mnyororo wa ununuzi zinapaswa kufuatiliwa kwa makini ili kuzuia upotevu wa fedha, uzembe na ukosefu wa uwajibikaji, mambo ambayo huathiri utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
“Kama hatutasimamia vizuri hatua hizi kutoka kupanga hadi kufikisha huduma tutapoteza fedha nyingi na miradi haitawanufaisha walengwa. Ndiyo maana tunawahitaji wahariri kuwa mabalozi wa elimu hii,” ameongeza.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa kikao hicho, Ben mwang'onda, alitoa wito kwa waandishi na wahariri kuandika habari za uchunguzi zenye lengo la kufichua mianya ya upotevu wa fedha na pia kuonyesha mafanikio ya matumizi sahihi ya rasilimali.
“Kwa kushirikiana, tunaweza kuhakikisha kuwa fedha za umma zinatumika kuleta maendeleo endelevu. Tunahitaji habari zenye kuelekeza suluhisho na si malalamiko tu,” amesema Mwangonda.
Warsha hiyo ni sehemu ya juhudi za serikali kuimarisha usimamizi wa fedha za umma na kutekeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs), hususan Lengo la 16 linalohusu kujenga taasisi madhubuti, zenye uwazi na uwajibikaji kwa wote.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...