NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
KLABU ya Yanga imeibuka mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara (NBCPL) baada ya kufanikiwa kushinda mechi yao ya kiporo dhidi ya mahasimu wao Simba Sc ambao nao walihitaji ushindi kwenye mchezo huo ili waweze kuwa mabingwa.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa vute ni kuvute, Yanga iliweza kuukamata mchezo katika kipindi cha kwanza licha ya kutopiga shuti kwenye lango la wapinzani hivyo kufanya mchezo kwenda hadi mapumziko matokeo yakiwa 0-0.
Pacome Zouzoua ndiye tunaweza kusema ndio mchezaji bora wa mechi maana ndiye aliyeukamata mchezo na kuwapa shida wapinzania kwani ndiye aliesababisha penati ambayo alikwenda kupiga na kufunga bao la kwanza.
Mabadiliko walioyafanya Yanga kipindi cha pili kwani Clement Mzize aliingia na kufunga bao safi akipokea pasi nzuri kutoka kwa nyota yule yule Pacome Zouzoua na kufanya matokeo kuwa 2-0 dakika 90 za mchezo.
Huu ni ubingwa wa nne mfululizo wa Yanga ligi kuu kuuchukua.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...