Zaidi ya wafanyabiashara 3,000 kutoka Tanzania na wengine zaidi ya 3,000 kutoka Uingereza wamejisajili kwenye Tanzania Link Portal, jukwaa la kidijitali linalolenga kuimarisha fursa za kiuchumi kati ya Tanzania na Uingereza kupitia ushirikiano wa biashara, uwekezaji, elimu, utalii na ajira.

Tanzania Link ni ubunifu wa Watanzania watatu wanaoishi Uingereza,  Bw Goodluck Mboya, Bw Joseph Ndilla, na Bi Shivani Patel, walioanzisha jukwaa hili kwa lengo la  kusaidia kufungua milango ya ushirikiano kwa Watanzania walioko nyumbani na wale waishio diaspora pamoja na washirika wao kutoka Uingereza.

Tovuti hiyo, https://www.tanzanialink.co.uk ilizinduliwa rasmi mwezi Aprili 2025 na Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, katika hafla maalum jijini London, Uingereza. Uzinduzi huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Bw Mbelwa Kairuki, Mama Mariam Mwinyi, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Bw Cosato Chumi, Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Bw Mizengo Pinda, pamoja na wanadiaspora na wadau wa maendeleo kutoka sekta mbalimbali.

Fursa Zilizopo Kupitia Tanzania Link

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Biashara wa Tanzania Link, Bw Joseph Ndilla, alisema jukwaa hilo limepokelewa kwa muitikio mkubwa, na tayari baadhi ya wafanyabiashara kutoka Tanzania na Uingereza wameanza mazungumzo ya ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji.

 “Kupitia Tanzania Link, tunawawezesha wafanyabiashara kupata taarifa na kushiriki katika fursa za uwekezaji wa moja kwa moja, ubia wa kibiashara, masoko ya kimataifa, na hata nafasi za ajira katika sekta mbalimbali. Pia tunasaidia Watanzania kupata taarifa sahihi kuhusu udhamini wa masomo (scholarships) na programu za ubadilishanaji wa kitaaluma na kielimu,” alisema Bw Ndilla.

Aidha, alisema Tanzania Link inatoa mwongozo na msaada wa kisheria kwa wafanyabiashara wapya, wajasiriamali, na wawekezaji wanaotaka kufanya kazi kati ya Tanzania na Uingereza, huku jukwaa hilo likitoa taarifa za utalii wa Tanzania Bara na Zanzibar kwa wageni kutoka Uingereza.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Ufundi, Bw Goodluck Mboya, alieleza kuwa Tanzania Link siyo tu jukwaa la kidijitali bali ni daraja la kimkakati linalounganisha watu, fikra na mitaji.

“Tanzania Link ni jukwaa la kizalendo lenye mtazamo wa kimataifa. Ni ishara ya mshikamano wa Watanzania duniani kote katika kujenga uchumi jumuishi. Tunachangia kwa vitendo utekelezaji wa diplomasia ya kiuchumi inayoasisiwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema Bw. Mboya.

Kwa upande wake, Balozi wa Tanzania Uingereza, Bw Mbelwa Kairuki alisema kuwa Tanzania Link ni jukwaa linaloendana na malengo ya kisera ya serikali ya kukuza diplomasia ya uchumi na ushirikiano wa kimataifa. 

“Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza unalipokea kwa mikono miwili na utaendelea kushirikiana kwa karibu na waanzilishi wake ili kuhakikisha mafanikio ya jukwaa hili kwa manufaa ya Watanzania na washirika wao wa maendeleo,” alisema Balozi  Kairuki.

Rais wa Zanzibar, Dkt Hussein Ali Mwinyi (wa tatu kushoto waliokaa) katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa tovuti ya https://www.tanzanialink.co.uk ambayo ni daraja la fursa mbalimbali kwa  Watanzania na Waingereza. Wa kwanza kushoto waliokaa ni Mama Mariam Mwinyi, mke wa Rais Mwinyi, Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Bw Mbelwa Kairuki, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Cosato Chumi (wa pili) kulia) na Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Mizengo Pinda.waliosimama kutoka kushoto ni  timu ya Tanzania Link, Bw Goodluck Mboya, Bi Shivani Patel, na Joseph Ndilla.

Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa Tanzania Link, Mkurugenzi wa masoko wa Tanzania Link, Bw Courtney Hayden (wa kwanza kushoto),  Mkurugenzi wa uendeshaji na mikakati  Bi Shivani Patel ( wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Biashara, Bw Joseph Ndilla (wa pili kulia) ja Mkurugenzi wa Ufundi, Bw Goodluck Mboya (wa kwanza kulia).

Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa Tanzania Link na maofisa wengine waliomtembelea nyumbani mwake, Migombani, Zanzibatr.

Wageni mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa tovoti ya ya https://www.tanzanialink.co.uk ambayo ni daraja la fursa mbalimbali kwa  Watanzania na Waingereza.

Maofisa wa Tanzania Link wakiwa katika picha ya pamjana ofisa wa kituo cha uwekezaji Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...