Na Mwandishi Wetu

MSANII wa muziki wa Bongo Flavor pamoja na filamu nchini Agness Suleiman 'Aggy Baby' ameibuka mshindi wa tuzo mbili tofauti kupitia shindano la Africa Arts Entertainment Awards (EAEA) 2025 zilizotolewa Julai 25, Jijini Dar es Salaam.

Mrembo huyo maarufu mwenye vipaji lukuki katika tasnia ya sanaa nchini na ushawishi mkubwa katika jamii, amepokea tuzo hizo Julai 25 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Aggy Baby tukio la tuzo hizo kwake linakuwa muendelezo wa tuzo mbalimbali anazoendelea kutunukiwa kwani mwaka 2024 pia alitunukiwa tuzo zingine

Hiyo inamfanya kuweka historia mpya katika tasnia ya burudani na maendeleo ya jamii baada ya kutangazwa mshindi wa tuzo hizo kubwa zilizokuwa zikiwaniwa pia na watu mbalimbali wakiwemo wasanii wa ndani na nje ya Tanzania.

Aggy Baby ameshinda katika vipengele viwili vinavyothibitisha mchango wake mkubwa ndani na nje ya sanaa ikihusisha tuzo za Best Inspirational Youth Icon / Motivator,Fastest Rising Foundation of Excellence iliyotolewa kupitia taasisi yake ya kijamii iitwayo 'Tupaze Sauti Foundation' ikihusika zaidi na utatuzi wa changamoto za makundi tofauti ya jamii wakiwemo wanawake na watoto.

Ushindi huo unathibitisha jitihada anazozifanya katika Muziki na Burudani, sambamba na kwenye eneo la kuhamasisha maendeleo kwa vijana wa Kitanzania kupitia elimu, ushiriki wao katika miradi mbalimbali ya kijamii pamoja na suala zima la maadili.

Akizungumzia Ushindi huo Aggy Baby kwake zimezidi kumpa chachu na nguvu zaidi ya kuendelea kupambana katika kila nyanja ili kujiongezea fursa zaidi za mafanikio sambamba na kuutangaza Tanzania.

"Namshukuru Mungu kwa hatua hii, kwangu ni faraja kubwa sana kupata ushindi wa tuzo hizo, inanifanya nijisikie faraja kubwa kwani ni wengi waliojitokeza kuwania ila Mungu imempendeza Mimi niwe mshindi" amesema Aggy Babby

Kwasasa Aggy Baby ni nembo ya ubunifu, kipaji na uzalendo wa kweli.Amewaomba mashabiki wake na Watanzania kwa ujumla kuendelea kumuunga mkono ili azidi kufanya kazi nzuri zaidi sanjari na kuifikia jamii kupitia taasisi yake ili kuleta matokeo chanya zaidi

Aggy Baby pia amekuwa ni kielelezo cha matumaini, uthubutu na mabadiliko chanya kwa kizazi kipya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...