Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan imekamilisha ujenzi wa shule mbili za kisasa za Amali Wilayani Kibondo Mkoani Tabora na Wilaya ya Mlele mkoani Katavi zinazogharimu Shilingi Bilioni 3.2

Vilevile serikali imetumia kiasi cha shilingi Bilioni 8.8 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa shule ya wasichana Rukwa iliyopo Wilayani Sumbawanga na Shule ya wasichana Katavi iliyopo Wilayani Nsimbo ambazo zote kwa pamoja zimeanza kutumika ili kuimarisha sekta ya elimu katika mikoa hiyo sambamba na nchi kwa ujumla wake.

Shule hizo zimejengwa kupitia Mradi wa kuboresha Ubora wa Elimu Sekondari (SEQUIP) ikiwa ni eneo muhimu la utekelezaji wa ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 kuhusu kuboresha sekta ya elimu nchini.

Miundombinu iliyojengwa kwa ajili ya shule za wasichana Katavi na Rukwa ni pamoja na maabara za (Kemia, Fizikia, Baiolojia na Jografia), vyumba vya madarasa na ofisi, Vyoo, mabweni, nyumba za walimu, Jengo la utawala, Bwalo, Jengo la TEHAMA, Mashimo ya maji taka pamoja na fensi.

Kwa upande wa Ujenzi wa shule mpya za Amali katika Wilaya ya Mlele mkoani Rukwa unahusisha ujenzi wa Madarasa na ofisi, Maktaba, Jengo la Utawala, Maabara za Kemia na Baiolojia, Jengo la TEHAMA, Mabweni 4, Bwalo la chakula, Karakana 2 za ufundi, Nyumba ya mwalimu, na Matundu ya vyoo.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...