Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kitaanza kubadilishana wafanyakazi na wanafunzi pamoja na kushirikiana katika tafiti na Chuo Kikuu cha Lala Lajpat Rai cha Tiba ya Wanyama na Sayansi za Afya cha Haryana, India hiyo ni baada ya hafla ya kusaini hati ya makubalinao ya kushirikiana yaliyosainiwa leo Julai 11, 2025 Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza baada ya tukio hilo, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo – Utawala Prof. Amandus Muhairwa amesema wamekuwa wakitembeleana na kufanya mazungumzo tangu mwaka 2023 kabla ya kufikia hatua hii ya kusaini makubaliano, yaliyotajwa kuwa chachu katika kuinua uwezo, maarifa na ujuzi wa wataalamu katika kukabiliana na magonjwa ya wanyama ambayo kwa kiasi kikubwa yanafanana baina ya mataifa hayo mawili.
Amesema ushirikiano huo ni juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kudumisha umoja na ushirikiano na taifa la India na kuongeza kuwa teknolojia ambayo imekuwa ikitumika India katika tiba ya wanyama, wataalamu wataongeza maarifa huko na watakuwa kwenye nafasi ya kujifunza na kurejea nchini wakiwa na uwezo mkubwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...