Na Said Mwishehe,Michuzi TV
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Aretas Lyimo ,amesema Mamlaka hiyo imebaini kuwa kuna baadhi ya wahalifu wa Dawa za kulevya wameanza kutumia mbinu ya kutumia maiti za binadamu kubeba dawa za kulevya huku ikibaini kuwa raia wa kigeni wanaongoza kuwatumia watanzania kusafirisha na kusambaza dawa za kulevya.
Ameyasema hayo leo Julai 9, 2025 Jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa kuhusu udhibiti na kupambana na dawa za kulevya nchini kwa kipindi cha Mwezi Mei hadi Julai, 2025.
"Mamlaka imebaini kuwa kwa sasa madawa hayo yanasafirishwa kupitia maiti hususani maiti kupasuliwa kichwa na kuondoa ubongo na kisha madawa hayo kuwekwa kwa ajili ya kusafirishwa". Amesema Kamishna Jenerali Lyimo.
Amesema kumekuwa na matukio ya raia wa kigeni kuwatumia watanzania kusafirisha au kusambaza dawa za kulevya.
"Mara nyingi, huanzisha mahusiano ya kirafiki na kisha kuUwahusisha katika biashara hii haramu kwa kutumia kampuni zao na vyombo vyao vya usafiri hususani bodaboda, bajaji, Tax na wasambazaji wa vifurushi". Amesema
Aidha amesema kuwa kumekuwa na matukio ya raia wa kigeni kuwatumia watanzania
kusafirisha au kusambaza dawa za kulevya. Mara nyingi, huanzisha mahusiano ya kirafiki na kisha kuUwahusisha katika biashara hii haramu kwa kutumia kampuni zao na vyombo vyao vya usafiri hususani bodaboda, bajaji, Tax na wasambazaji wa vifurushi.
Kamishna Jenerali Lyimo amesema katika operesheni kwa kushirikiana na yombo vingine vya dola, katika maeneo mbalimbali nchini na kukamata dawa za kulevya jumla ya kilogramu 37,197.142.
Amesema dawa hizo zinajumuisha, kilogramu 11,031.42 za dawa mpya za kulevya (New Psychoactive Substance) aina ya Mitragyna Speciosa, bangi kilogramu 24,873.56, mirungi kilogramu 1,274.47, skanka kilogramu 13.42, heroin kilogramu 2.21 na methamphetamine gramu 1.42.
Pamoja na hayo amesema ukamataji huo umehusisha dawa tiba zenye asili ya kuievya aina ya ketamine kilogramu 1.92, Fluni-trazepam (rohypnol) vidonge 1000, lita 6 za kemikali bashirifu aina ya hydrochloric acid na uteketezaji wa ekari 1.045.5 za mashamba ya bangi.
Vilevile, kilogram 26 za dawa za kulevya aina ya heroin, zilizokuwa ziingizwe nchini kutokea nchini Msumbiji zilizuiwa.
Amesema watuhumiwa 64 walikamatwa wakihusishwa na dawa hizo.






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...