Bodi ya Bima ya Amana (DIB) imewahimiza wananchi waliokuwa wateja wa benki zilizofungwa kutokana na kufilisika kujitokeza ili kuwasilisha madai yao ya fidia, huku ikibainisha kuwa kiasi cha shilingi bilioni 9.07 tayari kimelipwa kwa wateja wanaostahili.
Fidia hiyo inawakilisha asilimia 75.76 ya madai yote yaliyowasilishwa hadi Machi 2025 kwa wateja wa benki saba ambazo ni FBME Bank, Covenant Bank, Benki ya Ushirika ya Wakulima wa Kagera, Meru Community Bank, Mbinga Community Bank, Njombe Community Bank na Efatha Bank.
Akizungumza katika Maonesho ya 49 ya Sabasaba jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa DIB, Bw. Isack Kihwili alieleza kuwa waliobaki ni wale ambao bado hawajawasilisha madai yao licha ya kustahili kulipwa.
“Wateja zaidi ya asilimia 75 tayari wamelipwa fidia. Tunaendelea kuwahimiza waliobaki kujitokeza ili haki yao ipatikane,” alisema Bw. Kihwili.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa, FBME Bank imeongoza kwa kiasi cha madai yaliyolipwa kwa asilimia zaidi ya 57, huku benki nyingine zikifuatia kwa viwango vya juu pia – mfano Covenant Bank (83.73%), Kagera (94.06%), Meru (92.35%), Mbinga (84.66%), Njombe (87.26%) na Efatha.
Bw. Kihwili alisisitiza kuwa DIB imeendelea kuimarika ambapo hadi Desemba 2024, ilikuwa na mtaji wa zaidi ya shilingi trilioni 1.3, na taasisi 42 za kifedha tayari zimejiunga na kuchangia asilimia 0.15 ya amana zao kila mwaka.
Aidha, kiwango cha juu cha fidia kwa mteja mmoja kimeongezeka kutoka TZS 250,000 hadi TZS milioni 7.5 kufikia 2023, hatua inayolenga kulinda akiba za wananchi zaidi pindi benki inapofilisika.
Takwimu zinaonesha kuwa asilimia 99.24 ya wateja wote wa benki nchini wanalindwa kikamilifu na mfumo huu wa bima ya amana — kiwango kinachopita viwango vya kimataifa vya asilimia 90.
Hata hivyo, Bw. Kihwili alikiri kuwa zipo changamoto katika kushughulikia fidia za wateja wa benki zilizo na shughuli au ubia nje ya nchi kutokana na tofauti za mifumo ya kisheria.
Aliwahimiza wananchi kutembelea banda la DIB katika Maonesho ya Sabasaba ili kupata elimu ya kina kuhusu usalama wa fedha zao na namna mfumo wa bima ya amana unavyofanya kazi.
“Tunawahamasisha wananchi kuwa na uelewa wa haki zao kifedha. Kujua usalama wa fedha zako ni hatua ya kwanza katika kufanya maamuzi sahihi ya kifedha,” alisisitiza.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...