Kampuni ya Gf Trucks & Equipment Ltd imeibuka mshindi wa jumla wa maonyesho ya biashara ya kimataifa 2025 yanayoendelea jijini Dar es salaam.
Kupitia kiwanda chake cha kuunganisha Magari makubwa cha GF Vehicle Assemblers(GFA) kilichopo Kibaha mkoani Pwani
Katika maonesho hayo yalionza rasmi tarehe 28 mwezi wa sita yameshirikisha makampuni mbambali kutoka nje na ndani ya nchi Baadhi ya nchi ni China,Korea,Uturuki na kutoka Ulaya,Pia nchi za ukanda wa afrika ni miongoni mwa washiriki katika maonyesho hayo yaliokutanisha wafanyabiashara mbalimbali.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi ndiye aliyekua mgeni rasmi na kufanikiwa kutembelea mabanda kadhaa kabla ya kuanza kutoa tuzo na zawadi kwa washindi mbali mbali katika maonyesho hayo.
Mwinyi alitembelea banda la kampuni ya GF na kujionea bidhaaa mbalimbali zinazouzwa na kampuni hiyo, ambapo Magari madogo ya Hyundai,Mahindra ni miongoni mwa magari yanayouzwa katika kampuni hiyo
Magari makubwa aina ya FAW na Mashine na Mitambo ya XCMG pia alijionea jinsi michakato ya awali ya uunganishaji wa magari inavyofanya kupitia kiwanda cha kampuni hiyo cha GFA kilichopo Kibaha mkoani Pwani
Pia Mwinyi aliwapongeza GF kwa kuibuka kuwa vinara wa ma maonyesho hayo na kuwataka wasibweteke na kupanua zaidi katika uwekezaji na kuwataka wakaribie zanziba alimaliza Mwinyi
Akizungumza mara baada ya kupokea Tuzo hiyo ya ushindi wa jumla Mkurugezi wa kampuni ya GF ,Ali Karmali alisema wao kama GF wanajivuni kuwekeza nchini kama Kiwanda cha kwanza cha kutengeneza magari nah ii yote imetokana na mazingira mazuri ya Serikali kwa wawekezaji hivyo tunajivunia kuwa waongoza njia na makampuni mengine yajifunze kwetu akizungumzia kuhusu kiwanda hicho cha kuunganisha magari alisema wapo katika awamu ya tatu ya upanuzi itakayochukua zaidi ya wafanyakazi 3000 hivo kuongeza ajira kwa watanzania
Pia aliutoa ushindi huo kwa wafanyakazi kwani bila wao wasingeweza kufanikiwa,GF ni wauzaji wa Magari makubwa ya FWA,XCMG,HYUNDAI na mitambo ya kutengenezea barabara na sdhunguli za uchimbaji wa madini XCMG.
Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi akimkabidhi Mkurugenzi wa Kiwanda cha kuunganisha na kutengeneza magari nchini ya GFA, Ali Karmal tuzo ya mshindi wa jumla wa maonyesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa, jijini Dar es SalaamRais wa Zazibar ,Hussen mwinyi akimsikiliza mkurugenzi wa GF ,Ali Karmal wakati alipotembelea banda la kampuni ya GF kwenye maonyesho ya sabasaba
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...