Na Janeth Raphael MichuziTv - Dodoma

Serikali imeendelea kuboresha huduma za afya kwa kufanikiwa kupunguza vifo vya mama wajawazito na vifo vya mama na mtoto hali iliyochagizwa na kuanzishwa kwa Mfumo wa Rufaa wa M-Mama, uliosaidia wakinamama kujifungulia kwenye Vituo vya kutolea huduma za afya.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Kenani Kihongosi akizungumza na Watanzania kupitia mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita katika mkoa huo leo Julai 20, 2025 katika Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) jijini Dodoma.

“Vifo vya kinamama wajawazito vimepungua kwa asilimia 78 kutoka vifo 50 (2021) hadi vifo 11 (2025). Vifo vya watoto chini ya miaka mitano vimepungua kutoka vifo 859 (2021) hadi 117 (2025),” alieleza.

RC Kihongosi amesema Vituo vya kutolea huduma za afya vimeongezeka kutoka vituo 249 hadi vituo 350, sawa na asilimia 71.14.

Aidha, Hospitali mpya nane zimejengwa na kufanya jumla ya Hospitali kuwa 21 zikiwa na majengo ya kutolea huduma za dharura na vituo vipya vya afya 8 vimejengwa na kuufanya mkoa kuwa na vituo 66 na Zahanati mpya 38 zimejengwa na kuufanya mkoa kuwa na jumla ya Zahanati 350.

Kihongosi amesema, “kumekuwepo na upatikanaji wa huduma za kibingwa mpya 11 zilizoanzishwa ikiwemo; upasuaji, pua, koo na masikio, mifupa, magonjwa ya figo, magonjwa ya ngozi, uchunguzi wa magonjwa ya saratani, magonjwa ya uzazi na mtoto, magonjwa ya afya ya kisayansi, magonjwa ya ndani, watoto na mfumo wa mkojo.”

Aidha hali ya upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi imeongezeka kufikia asilimia 93 (2025) kutoka asilimia 65 (2021). Vile vile, mashine za kisasa zimesimikwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mount Meru, ikiwemo: CT-Scan, ECHO, ECG na MAMOGRAPHY.

Ameongeza kusema jumla ya watumishi 1,403 wameajiriwa na kufanya idadi ya watumishi wa afya kufikia watumishi 3,542 sawa na ongezeko la asilimia 66. Nyumba 105 za watumishi wa sekta ya afya zimeongezeka na kufikia nyumba 423, sawa ongezeko la asilimia 33.

RC Kihongosi amesema. “magari 14 ya huduma za dharura, magari tisa kwa ajili Timu za Uendeshaji Mkoa (RHMT) na Halmashauri (CHMT) pamoja na gari moja la huduma M-mkoba yamenunuliwa kwa ajili ya shughuli za usimamizi wa huduma za afya.”


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...