Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam. Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo, amewahimiza Watanzania kutumia kikamilifu fursa zinazopatikana katika sekta ya misitu ili kukuza uchumi, kulinda mazingira na kupambana na mabadiliko ya tabianchi.
Akizungumza jana Julai 7, 2025, katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF), Prof. Silayo alisema sekta ya misitu ni kiungo muhimu cha maendeleo kwa kuwa inachangia ukuaji wa sekta nyingine ikiwemo maji, nishati, kilimo na mifugo.
“Misitu ina nafasi ya kipekee katika kupunguza na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi. Kupitia maonesho haya, tunawaeleza wananchi umuhimu wa kuwa na misitu, kuhifadhi na kutumia fursa zilizomo ndani yake kwa maendeleo endelevu,” alisema Prof. Silayo.
Amesema sekta ndogo ya nyuki ni mfano wa jinsi uhifadhi wa misitu unavyoweza kuchochea kipato kwa wananchi kupitia ufugaji nyuki na uzalishaji wa asali, huku ikisaidia kulinda uoto wa asili.
Aidha, Kamishna huyo alisisitiza umuhimu wa uvunaji endelevu wa mazao ya misitu unaochochea ukuaji wa viwanda, hasa vya bidhaa za ujenzi na nishati safi, akibainisha kuwa TFS inaendelea kushirikiana na taasisi nyingine za serikali kutoa elimu ya upandaji miti na uhifadhi wa mazingira.
“Tunaelimisha wananchi kuhusu upandaji wa miti ya kibiashara, miti inayotunza vyanzo vya maji, matunda, dawa na miti kwa ajili ya kivuli mijini ili kukabiliana na hali ya hewa yenye mabadiliko ya mara kwa mara,” alisema Prof. Silayo.
Vilevile, alibainisha kuwa TFS inahamasisha uwekezaji katika utalii ikolojia kwa kutoa fursa kwa wawekezaji kuwekeza kwenye miundombinu ya malazi, michezo ya kitalii kama mbio za nyika, michezo ya magari na pikipiki pamoja na huduma nyingine zinazoweza kuongeza thamani ya misitu.
Prof. Silayo alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa mchango mkubwa wa kuutangaza utalii wa Tanzania kupitia filamu za kimkakati zilizowezesha dunia kufahamu vivutio vya nchi na hivyo kuongeza watalii na wawekezaji.
“Tunawaalika Watanzania na wawekezaji wa ndani na nje kufika TFS ili kushirikiana nasi katika kulinda, kuendeleza na kunufaika na sekta ya misitu. Misitu ni urithi wetu na mkombozi wa uchumi na mazingira,” alisisitiza Prof. Silayo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...