Na Diana Byera,Muleba
Timu ya Kasharunga FC imetwaa ubingwa na kujishindia kitita cha Shilingi Milioni 10 baada ya kuifunga Muhalila Cup All Starts kwa mikwaju ya penati 6–5 katika mashindano ya Kombe la Mia Mia yanayofanyika kila mwaka wilayani Muleba.
Mashindano ya Mia Mia yamehitimishwa kwa msimu wa 9 ambapo timu ya Muhalila Cup All Starts imejinyakulia Shilingi Milioni 5 kama mshindi wa pili, huku dakika 90 zikimalizika bila mbabe na mikwaju ya penati kufanya maamuzi ya kumpata mshindi.
Mwandaaji wa mashindano hayo, Sadath Yahya, alisema kuwa mashindano hayo yamekuwa chachu kwa vijana kuonyesha vipaji kwa miaka 9 mfululizo, huku wadau wanaotoa elimu ya sheria na wafanyabiashara wakiyatumia kama fursa ya kutangaza huduma zao kwa wananchi.
Alisema kuwa michuano hiyo ambayo imedumu mwezi mmoja ilizishirikisha timu 16, huku timu zote zilizoingia kuanzia robo fainali zikijipatia Shilingi Milioni moja moja, na zile zilizoishia hatua ya makundi zikijipatia jezi na mpira.
Moja ya changamoto aliyoitaja kama mdau wa michezo ni uwepo wa viwanja vichache ambavyo havikidhi mahitaji ya vijana wanaotaka kuonyesha vipaji katika wilaya hiyo.
Mdau wa michezo katika wilaya ya Muleba, Fortunas Muhalila, ambaye pia amekuwa akiandaa michuano ya Muhalila Cup, alisema kuwa wilaya hiyo inakumbwa na changamoto ya viwanja jambo ambalo linafifisha vipaji vya wachezaji.
Alisema serikali kwa kushirikiana na wadau wote wa maendeleo wakiweka nguvu katika michezo, huenda wilaya hiyo itazalisha vipaji halisi vitakavyoonekana kitaifa na kimataifa, huku akipongeza ubunifu wa wadau kuendelea kuanzisha mashindano ya mpira wa miguu katika wilaya ya Muleba.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, Issaya Mbenje, amepongeza ushiriki wa vijana katika fursa mbalimbali za wadau wanaojitokeza kuandaa mashindano ya michezo.
Alisema kuwa tayari Halmashauri ya Wilaya ya Muleba imebaini maeneo sita kwa ajili ya kutengeneza viwanja vya michezo mbalimbali, ambapo kwa mwaka huu wa fedha wametenga fedha kwa ajili ya kuanza utengenezaji ili vijana wapate sehemu salama ya kuonesha na kuendeleza vipaji vyao.
"Zamani ilikuwa ngumu kupata timu ya kutuwakilisha katika mashindano ya mkoa, lakini sasa tunashukuru wadau kwa kuendelea kugundua fursa za michezo na kubaini vipaji vya vijana. Sisi kama serikali tutakuwa na ninyi bega kwa bega katika maandalizi yote ya michezo na tutatatua changamoto za viwanja vya kuchezea," alisema Mbenje.
Mdhamini mkuu wa mashindano hayo kutoka shirika la msaada wa kisheria la Muhola, Sauro Marahuri, alisema mashindano hayo yamekuwa yakitumika kuhamasisha jamii kuachana na vitendo vya kikatili na kuwapatia wananchi huduma za msaada wa kisheria.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...