MASHINDANO ya Gofu kwa ajili ya kumuenzi mchezaji wa zamanı wa timu ya taifa ya wanawake ya gofu, marehemu Lina Nkya msimu wa nne yameanza kurindima rasmi leo katika Viwanja vya Lugalo Gofu jijini Dar es Saaalm.

Jumla ya wachezaji 150 wakiwemo 68 wa kulipwa na chipukizi na 82 wachezaji wasindikizaji wamesajiliwa kushiriki mashindano hayo ambayo yameanza leo Julai 17 na yatamalizikia Julai 20 mwaka huu katika viwanja hivyo.

Shindano hilo limeandaliwa na familia ya Said Nkya kwa lengo la kumuenzi mchezaji huyo Lina ambaye alikuwa ni miongoni mwa wachezaji waliopeperusha vyema bendera ya Tanzania mwaka 2011 walipotwaa taji la Afrika Mashariki na Kati katika mashindano ya Afrika Mashariki yaliyofanyika Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi, mratibu wa mashindano hayo Ayne Magombe amesema mashindano hayo yameanza leo na yanatarajiwa kumalizika Julai 20, 2025 na kwamba yanafanyika kila mwaka kwa kujumuisha klabu za wachezajii wote wanaopenda kushiriki mchezo huo kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Magombe amesema wapenzi wote wa mchezo huo wa gofu hasa waliopo Dar es Salaam wajitokeze kwa wingi kushirkki kwani ni moja ya fursa ya kuendelea kukuza na kuboresha ubora wao katika mchezo huo.

“Mashindano ya Lina Tour ni endelevu, kwa sasa tuna mashindano matano kwa mwaka, lakini tukipata sapoti kwa wadau wengine tunaweza kuwa na mashindano mengi zaidi ili kukuza huu mchezo,” amesema Magombe

Naye Mchezaji wa Gofu kutoka klabu ya Kilimanjaro, Racheal Mushi amesema amejipanga vizuri kwa ajili ya mashindano hayo na anamatarajio makubwa ya kuhakikisha kuwa anaibuka mshindi.

Amesema Lina PG Tour nii mnzuri kwani yanawaleta pamoja wachezaji mbalimbali hivyo amewaomba waandaaji wa mashindano hayo kuendelea kuandaa michuano hiyo ambayo ina lengo la kukuza vipaji katika mchezo wa gofu nchini.

“Niwaombe waandaaji waendelea kutuandalia michuano hii mizuri kwa sasa Tanzania lakini pia niwatake vijana kujitokeza kwa wingi kushiriki ili kuweza kukuza vipaji tulivyokuwa navyo,” amesema

Kwa upande wa baadhi ya wachezaji wa kulipwa wa gofu kutoka klabu ya Gymkhana Dar es Salaam na Lugalo wamesema wamejiandaa vizuri kushiriki michuano hiyo na wanaamini wataibuka washindi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...