Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma
Mawakili Nchini Tanzania wametakiwa kwenda kuzisoma sheria za Uchaguzi Mkuu, ili waweze kuwasaidia kujaza fomu wagombea waliojitokeza kutia nia, lakini pia kutatua migogoro itakayowasilishwa kwa kukosa uelewa katika Mahakama mbalimbali hapa nchini.
Jaji Mkuu wa Tanzania ,George Masaju ameyazungumza hayo leo jijini Dodoma wakati akiwathibitisha na kuwapokea Mawakili 449 wakiwemo wa Serikali na kujitegemea,ikiwemo kuorodheshwa rasmi katika orodha ya mawakili waliothibitishwa hapa nchini.
Aidha amewataka Mawakili hao kwenda kufanya kazi katika mikoa mingine tofauti na Dar es Salaam na Dodoma ambayo ina mawakili wa kutosha,ili kuepuka kuitwa vishoka hasa ukizingatia soko la Kada hiyo ni kikubwa kwa sasa.
Amesema kuna sheria nyingi na mbalimbali,zikiwemo za Polisi,uchaguzi na nyingine hivyo,Mawakili hao wanapaswa kutumia muda mwingi kuzisoma na kuzielewa ili waweze kutumia fursa za kuwasaidia wagombea mbalimbali waliojitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.
"Najua kazi zetu nyingi tunazipata kupitia kutatua migogoro mbalimbali hivyo tuweke jitihada ya kuzisoma sheria ili tuzielewe maana kuthibitishwa,kupewa vyeti na utendaji ni vitu viwili tofauti,"alisema Jaji Mkuu Masaju.
Kutokana na hilo aliwataka Mawakili kwenda kukiishi kiapo walichoapa na kukifanyia kazi ipasavyo,wasome sheria kila mara kwa sababu hubadilika,ili waweze kuisaidia jamii kwa ujumla katika maeneo ambayo watakwenda kuwajibika hapa nchini.
"Sisi tuliojaa hapa wakati mnapewa kiapo hatujaja kuwashangilia tumekuja kushuhudia kiapo chenu kama mtakwenda kukiishi kama Sheria inavyoelekeza,"alisema Jaji Mkuu.
Jaji Masaju akizungumzia kuhusiana na Mawakili hao kupenda kuishi kwenye miji mikubwa kama Dar es Salaam na Dodoma,alisema kitendo hicho kinamchukiza sana kwa sababu kuna maeneo mengi ambayo yana migogoro hivyo waende sehemu hizo wakawatumikie wananchi.
Akitolea mfano Wilaya ya Kilombero ambako kuna mashamba ya miwa,kuna wakulima wengi pamoja na jamii ambayo inahitaji huduma ya sheria hivyo waende huko kuwatumikia wananchi badala ya kubaki kwenye miji mikubwa.
"Nisingependa kuona mnazunguka Dar es Salaam na Dodoma muonekane kama vishoka tawanyikeni mikoa mingine mkafanye kazi ya kutenda haki ili kuisaidia jamii,lakini staki kusikia mnauza utu wenu kwa kupewa badala ya kutenda haki,"alisema Jaji Mkuu.
Mbali na hilo amewasisitiza Mawakili hao kutouza utu wao kwa kupokea fedha na kubadili haki ya mtu mwingine kuipeleka sehemu nyingine kitendo hiko hakikubaliki kabisa kwenye maadili ya kazi na kuongeza yeye ni mlezi mzuri na mawakili hao ndio mara ta kwanza anawapa kiapo hivyo asingependa kuona wanakwenda kinyume na maadili.
Amesema kuwa wasitegemee kwenda kuishi kama wanasiasa wao wanapaswa kwenda kutenda haki ili kuendelea kuaminika mbele ya jamii na kuongeza kuwa kama kesi haiwezi anapaswa kumwambia mteja wake ukweli na sio kuchukua pesa yake bure.
"Msitende dhambi ya kuchukua fedha ya watu ilihali mnajua kesi huiwezi ni bora umwambie ukweli mteja,usiwaze kununua gari ndogo kwa pesa ya mteja ambayo unajua kesi hashindi,hata wewe hutafanikiwa kwa sababu hujui amehangaika vipi kuitafuta hiyo pesa ili akulipe.
Naye Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Chiganga Tengwa alisoma idadi ya mawakili waliopokelewa na kuthibitishwa huku akiwataka kufuata taratibu watakazoelekezwa.
Ongezeko la idadi hiyo ya Mawakili waliothibitishwa imefanya kufikia mawakili 13,446 ambao watakuwa wanafanya shughuli za uwakili katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...