Na John Mapepele

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Mohamed Mchengerwa amemtaka mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Barabara ya Banana – Kitunda – Kivule – Msongola na Kivule – Majohe Junction, barabara za Kiwalani na Migombani kukamilika mradi huo kwa wakati bila kutoa visingizio vyovyote kwa kuwa tayari Serikali imeshamlipa fedha zote.

Mhe. Mchengerwa ametoa kauli hiyo leo wakati akikagua mradi huo akiambatana na Mbunge wa jimbo la Ukonga Mhe. Jerry Silaa.

Amesema dhamira ya Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha kuwa miundombinu ya barabara zote nchini inakamilika ili ziweze kupitika katika kipindi chote cha mwaka.

Aidha, amefafanua kuwa kukamilika kwa ujenzi wa barabara utasaidia kuboresha maisha ya wananchi kwa kuwa shughuli za uchumi zutaimarika.

Amempongeza Mhe. Rais kwa kutoa fedha nyingi kutengeneza miradi mbalimbali ya barabara hapa nchini huku akizitaka Mamlaka za Mikoa na Wilaya kuwasimamia wa wahandisi wanaotekeleza miradi hiyo na wasisite kuwazingatia mikataba ya kazi hizo.

Akitoa maelezo ya mradi huo, Meneja wa TARURA Mkoa wa Dar es Salaam Mhandisi Geofrey Mkinga amesema ujenzi wa barabara ya Banana- Kitunda- Kivule –Msongola unafanywa kwa awamu 2 tofauti ya 1 & 2 Mkandarasi M/s JIANGXI GEO ENGINEERING.

Utekelezaji kwa awamu ya kwanza ya mradi unahusisha ujenzi wa barabara ya Kitunda – Kivule – Msongola yenye urefu wa km 9.95 na barabara ya Kivule – Majohe Junction km 2.79 unaotekelezaji unafanywa na M/s JIANGXI GEO ENGINEERING chini ya usimamizi wa Mhandisi Consultancy Ltd.

Amesema mradi unatekelezwa kwa fedha za Mkopo kutoka Benki ya Dunia, kwa gharama ya TSh 30.37 bilioni.

Aidha amesema malipo yaliyokwishafanyika hadi sasa ni TSh. 4.55 bilioni kama malipo ya awali.

Hadi kufikia leo, mradi umefikia hatua ya utekelezaji ya 10%, huku muda wa utekelezaji uliopita ukiwa ni 32%.


Ameongeza kuwa kazi zilizokamilika ni pamoja na uondoaji wa tabaka la juu la udongo usiofaa kwa kilomita 5, ujenzi wa msingi wa barabara (roadbed) kwa kilomita 4, uwekaji wa vifusi aina ya G3 kwa kilomita 3 na uwekaji wa vifusi aina ya G7 kilomita 4.

Kwa upande wautekelezaji wa awamu ya pili amesema Mradi unahusisha ujenzi wa barabara ya Banana -Kitunda yenye urefu wa km 3.95, barabara ya Migombani km 1.57, barabara na barabara za Kiwalani zenye urefu wa km 3.22.

Aidha amesema utekelezaji unafanywa na M/s JIANGXI GEO ENGINEERING chini ya usimamizi wa Mhandisi Consultancy Ltd.

Mradi unatekelezwa kwa fedha za Mkopo kutoka Benki ya Dunia, kwa gharama ya TSh 28.51 bilioni.

Amesema kazi zilizokamilika ni pamoja na kazi za Survey kwa kuweka mipaka na vipimo vya barabara zote.

Aidha, amesema changamoto iliyojitokeza katika mradi huo ni mvua nyingi zilizonyesha kuanzia Februari hadi Juni 2025, ambazo ziliathiri kuanza kwa kazi nyingi ndani ya muda uliopangwa na

uwepo wa wafidiwa katika kipande cha barabara ya Banana-Kitunda eneo la Kipunguni ambao bado hawajapokea malipo yao. (Ulipwaji wa fidia hiyo unafanywa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege-TAA ikiwa ni kupisha eneo la Uwanja wa Ndege).

Pamoja na kwa Packages zingine ambazo fidia yake bado haijafanyika ili kupisha kuanza utekelezaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...