
MRAJIS na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Dkt Benson Ndiege ametoa rai kwa Vyama vya Ushirika nchini kutafuta wateja wakubwa ndani na nje ya nchi na kuingia nao makubaliano ya kibiashara.
Ametoa rai hiyo alipotembelea Kijiji cha Ushirika kwenye Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es Salaam ambacho kimeunganisha Vyama vya Ushirika 13.
Amesema Vyama vinatakiwa kufanya biashara zaidi na kuacha kujikita zaidi katika utoaji wa huduma kwa wanachama au Vyama wanachama wake.
“Tafuteni masoko ya ndani na nje ya nchi kupitia warsha, kongamano, ziara na mikutano mbalimbali za kimataifa ili Ushirika uwe wa kibiashara zaidi na kufanya kuwa kipaumbele cha uwekezaji, endeleni kujipambanua ili Ushirika uwe wa kibiashara zaidi kama ambavyo tunahamasisha sasa kutafuta mitaji kupitia Benki ya Taifa ya Ushirika ili mzidi kufanya hizo biashara kwa weledi na kuwa na uwezo wa kukidhi Soko la ushindani” amesema Dkt Ndiege
Vile vile amevitaka Vyama vya Ushirika kuendelea kutumia fursa ya Maonesho ya Kimataifa ya Biashara kwa kushiriki kwa wingi kila mwaka ili waweze kujifunza, kujitangaza na kupata masoko, wawekezaji na kujua mahitaji ya Soko kabla ya kuanza shughuli za uzalishaji
Vyama alivyotembelea ni Chama Kikuu cha Ushirika Igembensambo, RUNALI, Lindi Mwamboa, WETCU, KACU, MILAMBO, WAMACU, Chama cha Ushirika CHAWAKIMU, Kilimanjaro Diary Cooperative joint enterprise, Survival Women Cooperative na Benki ya Ushirika Tanzania (CBT).







Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...