Muandaaji wa mbio za NBC Dodoma Marathon, Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) leo imeendelea na zoezi la utambulisho na kukabidhi jezi maalum na vifaa vitakazotumiwa na washiriki wa mbio hizo kwa mdhamini kwa mkuu wa mbio hizo kampuni ya GSM Group ambayo kupitia kampuni yake tanzu ya GSM Beverages inadhamini huduma ya maji na vinywaji baridi katika msimu huo sita wa mbio hizo.

Zaidi GSM Group kupitia taasisi yake ya GSM Foundation ni wafadhili muhimu katika agenda tatu ya mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Julai 27, mwaka huu jijini Dodoma ambazo ni kuendeleza mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi, kupanua ufadhili wa wakunga hadi kufikia wakunga 200 pamoja na kuanzisha mpango mpya wa kufadhili masomo ya wauguzi 100 kwa ajili ya watoto wenye changamoto za usonji (autism) nchini.

Kama ilivyokuwa kwa wadhamini wengine, zoezi la kuwatembelea na kuwakabidhi vifaa hivyo wadhamini hao, leo pia liliongozwa na Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya NBC Bw Rayson Foya, alieambatana na baadhi ya maofisa wa benki hiyo akiwemo Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano ya Umma wa benki hiyo Bw Godwin Semunyu na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi yam bio hizo Bi Tatiana Massimba.

Wakiwa Makao Makuu ya kampuni ya GSM Group jijini Dar es Salaam, maofisa hao wa NBC walipokelewa na wenyeji wao Mkurugenzi wa GSM Group, Bw Gharib Said Mohamed (GSM), Mkurugenzi wa Uwekezaji wa kampuni hiyo Mhandisi Hersi Said, Mkurugenzi Msaidizi wa kampuni hiyo, Bi Chenedzo Mupukuta pamoja na maofisa wengine waandamizi wa kampuni hiyo.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Bw Foya pamoja na kuishukuru kampuni ya GSM Group kwa kuwa mdhamini muhimu wa mbio hizo na hivyo kuwa sehemu ya harakati hizo za kijamii ambazo kwa msimu huu zinalenga kukusanya fedha kiasi cha Tsh Milioni 700 zitakazosaidia kufanikisha agenda hizo tatu.

“Tupo hapa kukabidhi vifaa hivi kwa uongozi wa GSM Group kama ishara ya kuheshimu na kutambua mchango wao kwenye mafanikio ya mbio hizi. Udhaminiwa wa GSM Group kwenye mbio hizi unahusisha usambazaji wa maji na vinywaji baridi kwa washiriki takribani 12,000 tunaowatarajia kwenye msimu wa sita wa mbio hizi.’’

“Zaidi GSM Group wameenda hatua nyingine zaidi ambapo kupitia Taasisi yao ya GSM Foundation wameamua kuwa sehemu ya wafadhili muhimu katika agenda zetu hizi tatu ambazo kimsingi zinagusa uhai wa mama zetu na watoto wakati wa kujifungua huku pia mwaka huu tikiangazia zaidi changamoto ya watoto wenye usonji (autism)’’ aliongeza Bw Foya.

Kwa upande wake Mhandisi Hersi, pamoja na kuishukuru benki hiyo kwa ushirikiano huo na jitihada zake katika kukuza sekta ya michezo nchini pamoja na kuokoa maisha ya wana jamii, alisema alisema ushirikiano huo unathibitisha jitihada na azma ya pamoja baina ya taasisi hizo mbili katika kukuza afya ya mama na ustawi wa jumla wa jamii.

"GSM Group tunafurahi kuwa mshirika mashuhuri wa benki ya NBC katika kufanikisha kusudi hili lenye nia njema kwa jamii tunayoihudumia. GSM Group tunaamini kwa dhati kuwa juhudi za pamoja ni muhimu katika kukabiliana na changamoto zinazokabili jamii zetu. Kwa kutumia ujuzi na rasilimali mbalimbali, tunaweza kuongeza athari yetu na kupanua wigo wetu. Hivyo tunawakaribisha washiriki wengi zaidi waje NBC Marathon kwa kuwa pia tumejipanga kuhakikisha tunakidhi mahitaji yao ya maji na vinywaji vingine baridi,’’ alisema.

Akizungumzia maandalizi ya mbio hizo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio za NBC Dodoma Marathon Bi Tatiana Masimba alisema mwitikio wa washiriki kutoka ndani na nje ya nchi ni mkubwa huku usajili wa mbio hizi ukiendelea kupitia tovuti ya www.events.nbc.co.tz ambapo washiriki wanatakiwa kuchangia kiasi cha TZS 45,000 kwa usajili wa mtu mmoja mmoja au 42,000 kwa usajili wa kikundi chenye idadi ya watu 30 au zaidi.

Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya NBC Bw Rayson Foya (wa pili kushoto) sambamba na  Mkurugenzi wa Kampuni ya GSM Group, Bw Gharib Said Mohamed (GSM) (katikati),  Mkurugenzi wa Uwekezaji wa kampuni ya GSM Group, Mhandisi Hersi Said (kushoto), Mkurugenzi Msaidizi wa kampuni ya GSM Group Bi Chenedzo Mupukuta na Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Mahusiano ya Umma Bw Godwin Semunyu (kulia) wakionesha jezi maalum kwa ajili ya mbio za NBC Dodoma Marathon zinazotarajiwa kufanyika Julai 27, mwaka huu jijini Dodoma wakati wa hafla ya makabidhiano ya jezi hizo iliyofanyika leo  jijini Dar es Salaam.

Maofisa wa benki ya NBC wakiongozwa na Mkurugenzi wa Fedha wa benki hiyo Bw Rayson Foya (wanne kushoto) pamoja na maofisa wa kampuni ya GSM Group wakiongozwa na  Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Bw Gharib Said Mohamed (GSM) (katikati), wakionyesha moja ya jezi maalum kwa ajili ya mbio za NBC Dodoma Marathon zinazotarajiwa kufanyika Julai 27, mwaka huu jijini Dodoma wakati wa hafla ya makabidhiano ya jezi hizo iliyofanyika leo  jijini Dar es Salaam.

Maofisa wa benki ya NBC wakiongozwa na Mkurugenzi wa Fedha wa benki hiyo Bw Rayson Foya (kushoto) pamoja na maofisa wa kampuni ya GSM Group wakiongozwa na Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Bw Gharib Said Mohamed (GSM) (alievaa kanzu), wakijipongeza wakati wa hafla ya makabidhiano ya jezi maalum kwa ajili ya mbio za NBC Dodoma Marathon zinazotarajiwa kufanyika Julai 27, mwaka huu jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Fedha wa benki ya NBC Bw Rayson Foya (kushoto) akijadili jambo na Mkurugenzi wa Kampuni ya GSM Group Bw Gharib Said Mohamed (kulia) wakati wa hafla ya makabidhiano ya jezi maalum kwa ajili ya mbio za NBC Dodoma Marathon zinazotarajiwa kufanyika Julai 27, mwaka huu jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Uwekezaji wa kampuni ya GSM Group Mhandisi Hersi Said (alieshika jezi) akionesha jezi maalum kwa ajili ya mbio za NBC Dodoma Marathon zinazotarajiwa kufanyika Julai 27, mwaka huu jijini Dodoma wakati wa hafla ya makabidhiano ya jezi hizo iliyofanyika leo  jijini Dar es Salaam. Wengine ni pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio za NBC Dodoma Marathon Bi Tatiana Masimba  (kushoto), Meneja Mawasiliano na Mahusiano ya Umma Benki ya NBC Bi Irene Peter (wa pili kulia) na Meneja Masoko wa Kampuni ya GSM Group Bi Rukia Yazid (kulia).

Mkurugenzi wa Uwekezaji wa kampuni ya GSM Group Mhandisi Hersi Said (alieshika jezi) akionesha jezi maalum kwa ajili ya mbio za NBC Dodoma Marathon zinazotarajiwa kufanyika Julai 27, mwaka huu jijini Dodoma wakati wa hafla ya makabidhiano ya jezi hizo iliyofanyika leo  jijini Dar es Salaam.

Kampuni ya GSM Group kupitia kampuni yake tanzu ya GSM Beverages inadhamini huduma ya maji na vinywaji baridi katika msimu huo sita wa mbio hizo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...