…Wamo Januari Makamba, Mpina, Gambo, Askofu Gwajima na Ole Sendeka 


Na Said Mwishehe,Michuzi TV

PANGA limewapitia!Hivyo ndivyo unavyoweza kuelezea baada ya Kamati Kuu ya Chama

Cha Mapinduzi(CCM) kuacha majina ya makada wake maarufu na ambao wamekuwa Wabunge waliojizolea umaarufu mkubwa nchini.

Katika majina ambayo yametangwazwa leo Julai 29,2025 Mjini Dodoma licha wagombea wengi kupitishwa katika kuwania nafasi ya kuwania ubunge lakini wakati huo huo majina mengi maarufu yameachwa.

Miongoni mwa majina ya Wabunge ambayo hakupitishwa na Chama hicho ili kuwa sehemu ya mchakato wa kuwania ubunge ndani ya Chama hicho ni Luhaga Mpina ambaye alikuwa Jimbo la kisesa na January Makamba aliyekuwa Mbunge Jimbo la Bumbuli.

Wengine ni Josephat Gwajima aliyekuwa Mbunge Jimbo la Kawe, Mrisho Gambo aliyekuwa Mbunge Jimbo la Arusha Mjini, Christopher Olesendeka aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Simanjiro.

Katika orodha ya Wabunge hao maarufu ambao hawakupenya katika mchujo huo pia yupo Pauline Gekul aliyekuwa Mbunge Babati Mjini, Lengai Olesabaya  aliyekuwa Mbunge Arumeru Magharibi, Stephen Byabato aliyekuwa Mbunge Bukoba Mjini, Anjelina Mabula aliyekuwa Mbunge Jimbo la Ilemela pamoja na  Seif Gulamali aliyekuwa Mbunge Jimbo la Manonga

Kuondolewa kwa majina hayo kumeibuka maswali kwa baadhi ya wadau huku kila mmoja akiwa na mtazamo wake lakini baadhi ya wananchi wakieleza kuwa CCM ni Chama makini hivyo kitakuwa na sababu za msingi ambazo zimesababisha Wabunge hao maarufu na wenye majina makubwa kuwekwa kando .

Hata hivyo kwa Askofu Gwajima aliyekuwa Jimbo la Kawe yeye alijukuta akiingia matatani ndani ya Chama hicho kutokana na kauli zake mbalimbali ambazo amekuwa akizitoa dhidi ya Chama chake ,Serikali na kwa viongozi wakuu katika nchini.

Kwa Luhaga Mpiga wa Jimbo la Kisesa naye siku za karibuni alijikuta akiijgia katika wakati ngumu baada ya kushindwa kusoma alama za nyakati wakati Rais Dk.Samia Suluhu Hassan akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Simiyu ambapo kauli zake zilisababisha Rais kumjibu mbele ya wananchi.

Hata hivyo Mpina amekuwa hana mahusiano mazuri na viongozi wa Wilaya na Mkoa wa CCM na huenda ikawa ni sehemu ya sababu za kuwekwa kando.Hata hivyo Chama hicho hakijatoa sababu za kuwa ha Wabunge hao. 



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...