Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) imewataka Watanzania kujisajili katika mfumo wa manunuzi wa kielektroniki wa NEST ili waweze kunufaika na fursa mbalimbali za zabuni zinazotolewa na Serikali, hususan zabuni za asilimia 30 zinazolengwa kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.
Akizungumza leo Julai 5, 2025 katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba, Mkurugenzi Mkuu wa PPRA, Denis Simba, amesema mfumo huo hauchagui uwezo wa mtu bali inaangalia vigezo vya muombaji hivyo Mtanzania yeyote mwenye sifa anaweza kuomba zabuni ya ununuzi serikalini.
"Mnatakiwa kuchangamkia fursa hizi kwa kujisajili kwenye mfumo huu wa NEST na kujiandaa kufanya biashara na serikali kwa uwazi na ushindani ulio sawa". Amesema
Aidha amewataka watanzania kufika katika banda hilo kwa ajili ya kupata elimu ya namna ya kujisajili na kuomba zabuni za serikali ambazo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...