NA EMMANUEL MBATILO, PWANI
HIFADHI ya Mazingira Asilia ya Uluguru kutoka mkoani Morogoro imefanya ziara ya mafunzo katika Hifadhi ya Mazingira Asilia ya Pugu Kazimzumbwi, kwa lengo la kuwajengea uwezo wadau wa utalii kutoka mkoa huo, sambamba na kuimarisha ushirikiano katika uhifadhi wa mazingira na kukuza utalii wa ikolojia.
Mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa shughuli zinazofanywa na Mfuko wa Hifadhi ya Milima ya Tao la Mashariki (EAMCEF), yenye lengo la kuwezesha shughuli endelevu za misitu na utalii wa ikolojia ili kulinda viumbe hai na kuinufaisha jamii inayozunguka maeneo hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 4, 2025 Kisarawe mkoani Pwani, Afisa Utalii wa Hifadhi ya Uluguru, Bi. Wahida Masambuli alisema kuwa washiriki wa ziara hiyo walijumuisha waendesha kampuni za utalii, waongoza watalii, pamoja na vikundi vya ngoma kutoka mkoani Morogoro.
“Lengo letu si tu kuwajengea uwezo wadau wetu, bali pia kuboresha ushirikiano kati ya hifadhi hizi. Mgeni anayezuru moja ya hifadhi anaweza kupata taarifa za hifadhi nyingine, hivyo kuhamasisha utalii wa ndani na nje ya nchi,” alisema Bi. Wahida.
Kwa upande wake, Mwanzilishi wa Pugu Hills Eco Culture Tourism, Bi. Sairis Lucia Bugeraha, alisema ziara hiyo imefungua fursa za kubadilishana maarifa kuhusu utalii wa kitamaduni na uhifadhi wa mazingira, ikiwa ni sehemu ya mchango kuelekea kufanikisha lengo la Taifa la kufikisha idadi ya watalii milioni tano ifikapo mwaka 2030.
“Pia mafunzo haya ni njia ya kukumbushana wajibu wetu wa kulinda mazingira na kuhakikisha jamii inanufaika, hasa vijana na wanawake kupitia ajira zinazotokana na utalii wa asili na kitamaduni,” aliongeza Sairis.
Muhifadhi Msaidizi kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Bi. Regina Mwakifuna, alitoa wito kwa wananchi kutembelea hifadhi ya Kazimzumbwi na kujionea mandhari ya kuvutia pamoja na utalii wa kitamaduni unaoambatana na nyimbo na ngoma za asili.
Aidha, mwanakikundi wa Safaris Theater, Vincent Nicholaus, aliomba serikali kuboresha miundombinu ya vituo vya utamaduni ndani ya hifadhi hiyo ili kuongeza weledi na kupanua vivutio kwa wageni.
Naye Meneja wa Safaris Rider Tour alisisitiza umuhimu wa serikali kuendelea kuitangaza hifadhi ya Kazimzumbwi, akieleza kuwa bado ni eneo jipya kwa masikio ya wageni wengi, hivyo kuhitaji juhudi zaidi katika kuitangaza ili kuvutia wageni zaidi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...