Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Access Tanzania Ndugu Protase Ishengoma pamoja na ujumbe aliombatana nao Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 08 Julai, 2025.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo Maalum ya ‘Power of 100 Women Award kutoka kwa Uongozi wa Access Bank Group kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Access Tanzania Ndugu Protase Ishengoma Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 08 Julai, 2025. Tuzo hii ambayo hutolewa kila baada ya miaka mitano inalenga kutambua na kusherehekea wanawake wa Kiafrika wanaotoa michango ya mageuzi kwa mataifa na jamii zao, kuhamasisha na kuhimiza kizazi kijacho cha viongozi Wanawake katika bara zima la Afrika. Pia kupaza sauti za Wanawake katika kuleta maendeleo endelevu ya Kiuchumi na kijamii barani Afrika.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Tuzo Maalum ya ‘Power of 100 Women Award mara baada ya kukabidhiwa Ikulu Jijini Dar es Salaam 08 Julai, 2025.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Ujumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Congo- Brazzaville Mhe. Denis Sassou Nguesso uliowasilishwa kwake na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Jean-Claude Gakosso, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 08 Julai, 2025.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...