Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan imekamilisha ujenzi wa shule ya kisasa ya wasichana Mwanza ambayo imejengwa katika Wilaya ya Magu.

Shule hiyo imejengwa kupitia Mradi wa kuboresha Ubora wa Elimu Sekondari (SEQUIP) kwa gharama ya shilingi Bilioni 4.1 huku ikiwa na miundombinu toshelevu.

Miundombinu iliyojengwa ni pamoja na maabara nne za (Kemia, Fizikia, Baiolojia na Jografia), vyumba 22 vya madarasa na ofisi 6, Vyoo matundu 23, mabweni 9, nyumba 5 za walimu, Jengo la utawala, Bwalo, Jengo 1 la TEHAMA, Mashimo ya maji taka pamoja na fensi.

Pia serikali kupitia mradi huo wa SEQUIP imetoa jumla ya Shilingi Bilioni 1.6 na tayari ipo katika hatua za ukamilishaji wa ujenzi wa shule mpya ya Amali katika kijiji cha Mhungwe kilichopo katika Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.

Ujenzi wa shule hiyo mpya unahusisha ujenzi wa Madarasa 8 na ofisi 2, Maktaba, Jengo la Utawala, Maabara 2 za Kemia na Baiolojia, Jengo la TEHAMA, Mabweni 4, Bwalo la chakula, Karakana 2 za ufundi Umeme na Uashi, Nyumba ya mwalimu, na Matundu 8 ya vyoo.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...