Songea_Ruvuma.
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Ruvuma limetangaza katizo la umeme litakalotokea katika Wilaya ya Songea siku ya Jumamosi, tarehe 2 Agosti 2025, kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni.
Taarifa hiyo imetolewa na Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa shirika hilo, Alan Njiro, ambaye amesema kuwa katizo hilo ni sehemu ya maboresho ya huduma za umeme katika mji wa Songea.
Kwa mujibu wa Njiro, kazi zitakazofanyika ni pamoja na kubadilisha nguzo za miti ambazo zimekuwa mbovu na kuweka nguzo za zege zenye uimara zaidi, ambapo miti inayoathiri usalama wa nyaya za umeme itakatwa ili kuhakikisha usambazaji wa umeme unafanyika kwa ufanisi na bila hatari kwa wananchi.
Ameyataja maeneo yatakayoathirika na katizo hilo ni pamoja na Soko Kuu la Songea, Hospitali ya Mkoa, Mahakama Kuu, Ofisi za Mkuu wa Mkoa na Wilaya, Magereza, Songea Girls, RMA, pamoja na maeneo ya makazi kama Ruvuma Juu, Kipera, Liwena, Mateka, Ndilimalitembo, Matogoro Minarani, Mahenge, Makambi, Chandamali, Unangwa, Seedfarm, Matogoro, Chemchem na Boys.
Amesema TANESCO inawaomba radhi wateja wake kwa usumbufu utakaojitokeza wakati wa utekelezaji wa kazi hizo muhimu, Shirika hilo pia limetoa shukrani kwa wateja wake kwa uvumilivu wao, likisisitiza kuwa maboresho haya ni sehemu ya juhudi za kuboresha huduma ya umeme katika Mkoa wa Ruvuma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...