Na Said Mwishehe,Michuzi TV

WATUHUMIWA sita wakiwemo raia wawili wa China ambao wamefahamika kwa majina ya Chein Bai na Qixian Xin wamekamatwa eneo la Posta jijini Dar es Salaam wakisafirisha dawa za kulevya.

Dawa za kulevya walizokamatwa nazo ni aina ya Methamphetamine gramu 1.42, dawa tiba zenye asili ya kulevya aina ya frunitrazepam (rohypnol) vidonge 1,000 na Ketamine zenye uzito wa Kilogramu 1.92.

Akizungumza leo Julai 9,2025 jijini Dar es Salaam Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya(DCEA) Aretas Lyimo amesema watuhumiwa hao wamekamatwa katika operesheni iliyofanyika eneo la Posta jijini Dar es Salaam.

“Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama tulifanya operesheni ambapo tumefanikiwa kuwakamata watuhumiwa sita wakiwemo raia wawili wa China wakiwa na dawa za kulevya eneo watuhumiwa sita,wakiwemo raia wawili wa China

“Dawa hizo walikuwa wamekuwa katika vitu ambavyo unaweza kudhani ni kitabu kumbe sio ila ndani yake wameweka dawa hizo.Tunatoa rai kwa wageni wanaokuja nchini kwetu wahakikishe wanafanya shughuli halali ambazo wamekuja kuzifanya badala ya kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

“Tutaendelea na operesheni na yeyote ambaye anajihusisha na biashara hii tutamtia hatiani.Hivyo nisisiteze wageni mlioko nchini fanyeni kazi halali zilizowaleta.

Aidha amesema kwamba kumekuwa na matukio ya raia wa kigeni kuwatumia watanzania kusafirishaau kusambaza dawa za kulevya.

Amefafanua mara nyingi, huanzisha mahusiano ya kirafiki na kisha kuwahusisha katika biashara hii haramu kwa kutumia kampuni zao na vyombo vyao vya usafiri hususani bodaboda, bajaji, Tax na wasambazaji wa vifurushi.

Hivyo basi, wananchi wanapaswa kuwa makini na kuchukua tahadhari kubwa hasa pale wanapotumwa au kupokea mizigo kutoka kwa watu wasiowafahamu vyema.

Akielezea zaidi kuhusu operesheni iliyofanywa na mamlaka hiyo Kamishina Jenerali Lyimo amesema pia kulikuwa na kilogram 26 za dawa za kulevya aina ya heroin, zilizokuwa ziingizwe nchini kutokea nchini Msumbiji zilizuiwa.Watuhumiwa 64 walikamatwa wakihusishwa na dawa hizo.

Pia katika operesheni iliyofanyika bandari kavu eneo la Temeke jijini Dar es Salaam, kilogramu 11,031.42 za dawa za kulevya aina ya Mitragyna speciosa zilizoingizwa nchini kutokea nchini Sri Lanka zilikamatwa zikiwa kwenye vifungashio vyenye chapa inayoonesha kuwa ndani yake kuna mbolea.

“Mitragyna speciosa iko katika kundi la dawa mpya za kulevya zinazotokana na mimea inayofahamika kwa jina la “Kratom” mmea huu unakemikali aina ya Mitragynine na 7-Hydroxymitragynine (7-HMG).

“Ambayo ainasifa ya vichangamshi (stimulants) na vipumbaza (depresants) vyenye madhara ya kiafya kwa mtumiaji kwani huathiri mfumo wa fahamu na kusababisha uraibu hata kupelekea vifo vya ghafla.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...