Na Mwandishi wetu- DODOMA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. William Lukuvi amefanya ukaguzi wa maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa yanayotarajiwa kufanyika tarehe 25 Julai 2025 katika Uwanja wa Mashujaa, Mtumba – Dodoma.


Maadhimisho hayo yatapambwa na gwaride kutoka majeshi matano ya ulinzi na usalama na mgeni rasmi atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Katika ziara hiyo, iliyofanyika leo tarehe 16 Julai, 2025 jijini Dodoma Waziri Lukuvi aliambatana na viongozi waandamizi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na maafisa kutoka JWTZ na Jeshi la Polisi.








Maandalizi yameelezwa kuendelea vizuri, huku tukio hilo likitarajiwa kuwa la Kitaifa na kihistoria katika kutoa heshima kwa mashujaa wa Tanzania.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...