Na Linda Akyoo.

Kampuni ya Zara Tanzania Adventures imefanikiwa kuzindua msimu wa tano wa kampeni ya "Twenzetu kileleni 2025" ambapo leo kuu ni kupanda mlima Kilimanjaro na kusheherekea miaka 64 ya uhuru wa Tanganyika.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika katika ofisi za Zara Tanzania Adventure Mjini Moshi, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu amesema kuwa kampeni hiyo imekuwa na mafanikio makubwa katika kuongeza idadi ya watalii.

“Hii kampeni imekuwa maarufu sana. Tunapata wageni wengi, lakini hatuna mahali pa kuwaweka. Wito wangu kwa Mkurugenzi Zainabu, kama fedha zipo, jenga hoteli nyingine. Watalii hawana mahali pa kulala, wanapata tabu kutoka Arusha kuja Kilimanjaro,” amesema Babu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Zara Tanzania Adventure, Bi. Zainabu Ansell amesema kampeni hiyo inatarajiwa kuwashirikisha zaidi ya watalii 200 mwaka huu, wote wakipanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kusherehekea uhuru wa nchi.

Naye Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA), Anjela Nyaki, amepongeza mchango wa Zara Tanzania Adventure katika kukuza utalii na kuongeza mapato ya taifa kupitia idadi kubwa ya watalii wanaowaleta kila mwaka.

Zoezi hilo la kupanda Mlima Kilimanjaro linatarajiwa kufanyika kuanzia Desemba 5 hadi Desemba 10, 2025, likiwa pia ni sehemu ya kuendelea kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini, hususani Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro. Sambamba na hilo "Twenzetu Kileleni” msimu wa tano, inalengo la kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kusherehekea miaka 64 ya Uhuru wa Tanganyika.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...