Na Mwandishi Wetu

MGOMBEA wa nafasi ya udiwani Kata ya Makurumla iliyopo Magomeni mkoani Dar es Salaam kwa tıketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)Bakari Kimwanga amechukua fomu ya kugombea nafasi hiyo huku akiahidi kuendelea kushirikiana na wana Makurumla kukamilisha miradi ya maendeleo.

Akizungumza leo Agosti 19,2025 Bakari Kimwanga amesema wanachama wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) wakiongozwa na Mwenyekiti wa kata hiyo Idd Toatoa wamejitokeza kwa wingi kushiriki na kushuhudia akichukua fomu ya kugombea udiwani katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu.

“Tumekuja kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya udiwani ,hivyo tutaijaza na kurejesha kama utaratibu wa kisheria unavyoelekeza.Kubwa tunaamini wananchi wa Kata ya Makurumla wanamatumaini na kiu ya kutaka kujua kuhusu kasi ya maendeleo.

“Hivyo hivyo jambo moja tu la kuhaidi katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2020 hadi 2025 tuliahidi kufanya kazi ya kuleta maendeleo,kazi ambayo tumeifanya kwa kushirikiana na wananchi na sasa mwaka 2025 hadi mwaka 2030 tunakwenda kukamilisha.”

Kimwanga ametoa rai kwa wananchi kuendelea kukiamini Chama Cha Mapinduzi CCM na kukupa kura nyingi kwa Dk.Samia Suluhu Hassan ambaye ni mgombea Urais kwa tiketi ya Chama hicho,Mgombea ubunge Jimbo la Ubungo pamoja na Diwani wa kata ya Makurumla.

Amewaomba kuendelea kushirikiana kwa pamoja katika kuleta maendeleo ya kata hiyo na kwamba anaamini kwa ushirikiano ambao waliompatia mwaka 2020 hadi 2025 umemfanya awe na mataimani makubwa kubwa yale ambayo wamepanga kuyafanya kwa ajili ya maendeleo yatatekelezwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM kata ya Makurumla Idd Toatoa ametumia nafasi hiyo kuwashukuru WAN’a CCM na wananchi ambao wamejitokeza katika jambo hilo la uchukuaji fomu ya udiwani kwa Mgombea wao

“Tumemsikindikiza Mgombea wetu wa udiwani kata ya Makurumla Bakari Kimwanga,binafsi nimefurahi sana kwa siku ya leo kuja kuchukua fomu kwa ajili ya Mgombea Wetu.Wanachama wamejitokeza kwa wingi na tutaendelea hivi hivi katika kipindi chote cha kampeni na kufanikisha ushindi wa kishindo kwa mgombea Wetu wa Urais,Mbunge na Diwani.

Awali Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Kata ya Makurumla Abdallah Mnyuka amesema kuwa leo ndio ilikuwa siku yao ya kuchukua fomu ya udiwani kwa ajili ya mgombea wao na wana CCM wamejitokeza kwa wingi na hamasa ni kubwa kama kawaida yao.

“Mwaka 2020 katika Uchaguzi Mkuu Kata ya Makurumla ndio iliyoongoza kwa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kutoa kura nyingi kwa Rais ,Mbunge na Diwani na mwaka huu 2025 tunakwenda kuivunja rekodi yetu kwa kupata kura nyingi zaidi kwani hii ni kawaida yetu.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...