BANK of Africa Tanzania yashiriki katika maadhimisho ya miaka 26 ya Mfalme Mohammed VI wa Ufalme wa Morocco. Tukio hilo la lilifanyika jijini Dar es Salaam na kuwakutanisha viongozi wa kidiplomasia, mabalozi kutoka nchini mbalimbali wanaowakilisha nchini zao hapa Tanzania, wafanyabiashara, na wawakilishi mbalimbali katika kuadhimisha siku hiyo muhimu.
Bank of Africa Tanzania ni kampuni tanzu ya BANK OF AFRICA Group, mtandao wa kifedha wa Kiafrika wenye makao yake makuu nchini Morocco, ukiwa na mtandao katika nchi 17 za Afrika pamoja na pia nchini Ufaransa. BANK OF AFRICA – BMCE, benki ya pili kwa ukubwa miongoni mwa benki binafsi nchini Morocco.
Katika tukio hili, benki ilisisitiza tena dhamira yake ya kuimarisha uhusiano wa pande mbili kati ya Tanzania na Morocco kupitia ushirikiano wa kifedha na kitamaduni.
Maadhimisho haya yalidhihirisha uhusiano unaokua kwa kasi kati ya mataifa haya mawili, ambapo Bank of Africa Tanzania inachukua nafasi ya kiunganishi kati ya Afrika Mashariki na Afrika Kaskazini, kwa lengo la kuchochea ushirikiano wa kiuchumi na ustawi wa pamoja.
Bank of Africa Tanzania itaendelea kushiriki katika kuendeleza maendeleo ya kikanda kupitia ushirikiano wa kimkakati barani Afrika na kwingineko.
Mgeni rasmi alikuwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo (MP), Waziri Wa Mambo Ya Nje Na Ushirikiano Wa Afrika Mashariki

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiriano wa Afrika Mashariki Mh. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (MP) akiwasili katika hafla hiyo akipokelewa na Mh. Zakaria El Goumiri, Balozi wa Ufalme wa Morocco nchini Tanzania (kushoto)

Mkurugenzi wa Fedha wa Bank of Africa Group, Taha Bezzaz,(kulia) akisalimiana na Zakaria El Goumiri, Balozi wa Ufalme wa Morocco nchini Tanzania, (Kati kati) anayeangalia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji – Biashara wa Bank of Africa Tanzania, Hamza Cherkaoui katika maadhimisho ya 26 ya Mfalme wa Morocco yaliyofanyika jijini Dar es Salaam
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...