Benki ya Ushirika Tanzania (Coop Bank) imeingia makubaliano na Mfuko wa Pembejeo (AGTIF) yatakayowezesha benki hiyo kutoa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 8.5 kwa vijana wanaojihusisha na kilimo kupitia programu ya Jenga Kesho Iliyo Bora (Building a Better Tomorrow – BBT).
Akizungumza kwenye hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Coop Bank Godfrey Ng’urah alibainisha kuwa makubaliano hayo ni utekelezaji wa mpango mkakati wa benki hiyo unaolenga kuchangia ustawi kwa wote.
Kwa uoande wa AGTIF, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa AGTIF Itandula Gambalagi alisema Mfuko wa Pembejeo za Kilimo ulianzishwa chini ya Sheria ya Mfuko wa Pembejeo za Kilimo, Sura ya 401, Marekebisho ya 2002, kwa lengo la kupunguza pengo la usambazaji wa pembejeo kwa kufadhili uagizaji na usambazaji wa pembejeo za kilimo huku akibainisha kuwa taasisi yake imetoa mikopo wenye thamani ya bilioni 94 tangu kuaanzishwa kwake.
Naye, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Dr. Stephen Nindi ambaye alikuwa Mgeni Rasmi Katika hafla hiyo aliwasihi vijana na wanaushirika ambao watanufaika na mkopo huo kuweka taratibu za kuweka marajesho ili kuwezesha mkopo huo kuwa endelevu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...