Na Said Mwishehe,Michuzi TV
BODI ya Utalii Tanzania (TTB) imepokea kundi la wadau wakubwa katika sekta ya utalii kutoka nchini Urusi ambapo wadau hao watapata fursa ya kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo katika hifadhi za Taifa sambamba na kuangalia maeneo ya uwekezaji katika sekta hiyo.
Akizungumza Agosti 20,2025 jijini Dar es Salaam wakati wa Jukwaa la Uwekezaji kati ya Tanzania na Urusi , Mkurugenzi wa Utalii kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Thereza Mugobi aliyemwakilisha Waziri wa Wizara hiyo, Dk. Pindi Chana amesema ujio wa wadau hao ni sehemu ya utelekezaji wa maazimio ya Tume ya pamoja kati ya nchi hizo yaliyofanyika mwaka 2024.
Katika maazimio hayo ilielekezwa Bodi ya Utalii Tanzania kuandaa ziara ya mafunzo kwa wadau wa utalii kutoka nchi ya Urusi kutembelea Tanzania kwa ajili ya kuona shughuli mbalimbali zinazohusu utalii pamoja na kutembelea hifadhi zilizopo.
Dk.Mubogi ameeleza kuwa wadau hao wa utalii pia wataona maeneo ya uwekezaji ambayo Tanzania inaweza kuyatoa kwa ajili ya sekta ya utalii huku akifafanua kwamba kupitia TTB wametekeleza maazimio hayo kwa kuandaa Jukwaa hili la uwekezaji na kufanikisha ziara hiyo.
Akieleza zaidi Dk. Mugobi ambaye alımwakilisha Waziri wa Maliasili na Utalii aliyekuwa mgeni rasmi katika jukwaa hilo amesema miongoni mwa changamoto zilizojadiliwa kwenye maazimio hayo ni kuanzisha safari za ndege za moja kwa moja kutoka Tanzania hadi Urusi.
“Moja ya changamoto ambayo imeelezwa na ndugu zetu wa Urusi ni kwamba wanashindwa kuja Tanzania kwasababu hakuna ndege ya moja kwa moja kutoka kwao kuja nchini kwetu.
“Hivyo tayari Wizara ya Uchukuzi imeanza maandalizi ya kutekeleza jambo hilo na hatimaye kuwepo na ndege ya moja kwa moja kati ya nchi hizo kuvutia idadi ya watalii wanaotoka Urusi ambao wanatamani kutembelea Tanzania kuona vivutio vya utalii lakini changamoto ni usafiri.”
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Ephraim Mafuru amesema wamepokea wageni zaidi ya 35 kutoka nchini Urusi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mahusiano ya kidiplomasia yaliyoanzishwa baina ya nchi hizo.
“Lengo la Wizara ya Maliasiali na Utalii ni kuhakikisha mahusiano ya kidoplomasia yanatafsiri idadi ya watalii wanaokuja nchini, tunaamini kwamba nchi hiyo ni moja kati ya mataifa makubwa duniani yenye uwezo wa kifedha na idadi kubwa ya watalii, “amesema Mafuru.
Amesema TTB imejizatiti katika nchi ya Urusi kutangaza Utalii, wamewaleta wawekezaji wa daraja la kuu kutembelea vivutio ya utalii ikiwemo Hifadhi ya Ngorongoro na maeneo mengine watakuwa nchini kwa siku 10.
“Tunafanya hivi kujumuisha mazao mbalimbali ya utalii, ikiwemo Utalii wa Wanyamapori, fukwe, historia ili mgeni anapokuja aweze kuyaona yote haya na kupata uzoefu, hio ndio Tanzania tunayoitarajia tunaamini Warusi watakwenda kutangaza,” amesema Mafuru.
Awali Balozi wa Urusi nchini Tanzania Andrey Avetysyan amesema amesema nchi ya Tanzania imekuwa na vivutio vya kipekee ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika huku akieleza kuwa kuna wakati alikwenda Zanzibar ambapo alivutiwa na maeneo mengine mengi ya fukwe, na alipata mambo mapya.
“Nchi hii ni kubwa, na imejaa hazina, uzuri wa chochote unachotaka kuona.Katika sehemu nyingi barani Afrika, unaweza kwenda kwa safari, kama Afrika Kusini, lakini Tanzania ni mahali pa kipekee.”

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...