NA MWANDISHI WETU
MAMLAKA ya Masoko ya Mitaji na dhamana Tanzania (CMSA) imeipongeza Kampuni ya Vertex International Securities kwa ubunifu wa kuleta bidhaa mbili mpya sokoni zenye tija kwa Watanzania.

Vertex  imezindua leo  bidhaa hizo  jijini Dar es Salaam kwenye soko la mitaji ambazo ni Vertex bond fund na Vertes International Securities exchange Traded fubd (VIS-ETF).

Akizungumza katika hafla hiyo Mtendaji Mkuu wa (CMSA) CPA Nicodemus Mkama amesema, jambo walilolifanya Vertex ni kubwa na linatakiwa kuwa mfano wa kuigwa katika  kuyafanya masoko ya mitaji kuzidi kuleta matokeo chanya.

Mkama amesema masoko ya mitaji ya dhamana yanaendelea kutoa bidhaa bunifu kila siku na  bidhaa hii ni ya kwanza kwa kuungana na nchi nyingine kutoa bidhaa bunifu kama hiyo, hivyo Serikali inajukumu la kuendeleza na kusimamia masoko ili shughuli zifanyike kwa kufuata sheria, taratibu na miongozo ili kuleta uwazi na haki kwa washiriki wote.

"Vertex bond fund na VIS ETF zimekidhi matakwa ya kisheria na kupata idhini ya mamlaka ya masoko ya mitaji, uzinduzi huu unaashiria kuwa masoko ya mitaji nchini yanakuwa imara na kutoa bidhaa bunifu zinazowavutia wawekezaji wa ndani na wa Kimataifa, lengo kuu ni kutoa fursa mpya uwekezaji wa ndani na Kimataifa kwa watu binafsi, taasisi na wafanyabiashara,"amesema Mkama.

Aidha Mkama amesema mifuko hiyo itawawezesha wananchi kushiriki shughuli za kiuchumi na kuongeza vipato vyao jambo linalozidi kupanua wigo mpana na maendeleo ya uchumi, mifuko hiyo inawezesha utekelezaji wa dira ya Taifa pia.

"Uwekezaji huu ni wa kiwango cha chini kuanzia kipande kimoja kwa sh. 100 hadi vipande vitano yaani sh. 500 uwekezaji ambao unampa nafasi Mtanzania yoyote wa kipato chochote,"amesema Mkama.

Mtendaji wa Vertex International Securities, Mateja Mgeta, amesema lengo la kuletwa kwa bidhaa hizo sokoni ni kuwawezesha watanzania katika ujumuishi wa kifedha.

Amesema bidhaa hizo zitawafanya watanzania kuwekeza kwenye hatifungani kwa njia nyepesi na gharama nafuu "mfuko huu unatoa fursa kwa mtu mmoja mmoja kuanza kununua vipande vyenye thamani ya sh. 100 kila kimoja kiwango cha chini ikiwa ni vipande vitano vyenye thamani ya sh. 500,"amesema Mgeta.

Mgeta amesema hatua hiyo itakuwa rafiki na yenye manufaa makubwa kwa kuwa inalenga kuwafikia wananchi wote kwa ajili ya kujiwekea akiba kwa maendeleo ya sasa na baadae.

"Kupitia VIS-ETF Mtanzania anaweza kuwekeza kwa kiwango cha chini sh 20,000 na kwa kuanzia hisa hizi za VIS-ETF zitawekezwa kwenye hisa za CRDB Benk plc, NMB Bank plc, National investment coparation of Tanzania (NICO), DSE na AFRIPRISE,"amesema Mgeta.

Amesisitiza kuwa mifuko hiyo miwili inalenga sio tu kuongeza ushiriki wa wananchi katika masoko ya mitaji bali inaimarisha uchumi wa nchi kwa kutoa fursa ya ukusanyaji wa mitaji kwa ajili ya miradi yenye tija na kupanua uelewa wa Umma kuhusu uwekezaji wa pamoja.

Nae David Shambwe, Mkurugenzi wa Usimamizi wa Utendaji kwa Taasisi zisizo za Kibiashara katika Ofisi ya Msajili wa Hazina, amesema bidhaa hizo Mfuko wa Dhamana wa Vertex (Vertex Bond Fund) na Mfuko wa Uwekezaji wa Hisabe wa Vertex (Vertex Exchange Traded Fund - VIS ETF).

Amesema kuwa mifuko hiyo mipya imelenga kufungua fursa za uwekezaji kwa idadi kubwa zaidi ya Watanzania, hususan watu wenye kipato cha chini na jamii za vijijini.

“Kuna umuhimu wa kuwa na mjadala wa kitaifa kuhusu kuwahusisha watoto katika usimamizi wa mali, hasa baada ya wazazi kufariki dunia,” 

Emanuel Nyalali, Mkuu wa Maendeleo ya Biashara katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), alisema VIS ETF inapanua fursa kwa wawekezaji wa mapato ya kudumu na inaunga mkono jukwaa la kidijitali la uwekezaji la DSE.










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...