Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), CPA Habibu Suluo na Kamishina wa Mamlaka ya Usimamizi  wa Bima Tanzania (TIRA), Dkt. Baghayo Saqware, leo tarehe 8 Agosti, 2025, kwa nyakati tofauti wametembelea Banda la Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), lililopo kwenye Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa Nanenane mkoani Dodoma.

Wakiwa bandani walipewa maelezo kuhusu TASAC inavyosimamia suala la Mafunzo na Utoaji vyeti kwa mabaharia namna inavyochagiza masuala ya upatikanaji wa ajira kwa mabahari wa Kitanzania katika meli za kigeni.

Aidha walijulishwa kuhusu ujio wa boti mbili mpya za utafutaji na uokoaji ambazo zitatumika sambamba na boti ya kisasa ya matibabu ya dharura (Ambulance Boat) zilizopatikana kupitia Serikali ya Awamu ya Sita, kwa lengo la kuimarisha huduma za utafutaji na uokoaji katika Ziwa Victoria.

Kauli mbiu ya Maonesho hayo ni: "Chagua Viongozi bora kwa Maendeleo endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025", yalianza rasmi tarehe 01 Agosti, 2025 na yamehitimishwa leo tarehe 08 Agosti, 2025.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...