MKUU wa Wilaya ya Temeke, Sixtus Mapunda, amezielekeza halmashauri za manispaa zote mkoani Dar es Salaam, kuhakikisha zinawatumia kikamilifu wahitimu wa mafunzo ya awali ya Jeshi la Akiba katika utekelezaji wa operesheni mbalimbali.
Ametoa maelekezo hayo leo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, katika hafla ya ufungaji wa Mafunzo ya Awali ya Jeshi la Akiba Kundi la 63/2025 yaliyofanyika katika viwanja vya Kambi ya Jeshi la Wanamnchi Tanzania ya Twalipo, wilayani Temeke.
“Manispaa zote katika shughuli zao na operesheni zao ziwatumie vijana hawa. Wakurugenzi muwatumie wahitimu hawa haraka kabla hawajarudi mtaani,”amebainisha Mapunda.
Amesema vijana hao wakiachwa mtaani kwa kipindi kirefu bila kutumika watasahau kwa haraka kiapo chao.
“Tuna operesheniu za kukusanya mapato. Tuna maandalizi ya uchaguzi mkuu na kusimamia taratibu mbalimbali katika manispaa zetu. Hawa vijana wako tayari kutumika,”ameeleza Mapunda.
Aidha, ametoa wito kwa wahitimu hao kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29 mwaka huu.
“ Oktoba 29 ni siku ya uchaguzio mkuu. Tujitokeze kwa wingi kupiga kura. Ninawakabidhi jukumu la kwenda kuhamasisha vijana wenzenu kujitokeza kupiga kura,”amesema.
Mapunda aliwataka, aliwataka wahitimu hao kuishi kwa kiapo na kujiepusha kutumia mafunzo waliyopata katika vitendo viovu.
Awali Mshauri wa Jeshi la Akiba Mkoa wa Dar es Salaam, Kanali Emmanuel Kasyupa, alisema mafunzo hayo yalijumuisha vijana kutoka wilaya tano za mkoa huo ambazo ni Ilala, Temeke, Kinondoni, Kigamboni na Ubungo.
“Mafunzo yalianza Aprili nne mwaka huu yakiwa na wanafunzi 414. Wanafunzi 66 walishindwa kuendelea kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za utoro, matatizo ya afya na utovu wa nidhamu,”alieleza Kanali Kasyupa.
Amesema jumla ya wahitimu wote ni 348, wanaume 263 na wasicha 85 ambapo mafunzo hayo yalifanyika kwa wiki 18.
Kanali Kasyupa alibainisha, wakufunzi walitoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Jeshi la Polisi, Uhamiaji, Usalama wa Taifa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
“Kiapo kimesikika. Mmeahidi kuwa watiifu na waaminifu kwa Amirijeshi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mtakuwa watiifu kwa raia . Usiende kukiweka kiapo hiki katika begi. Ikiwezekana ubandike sebuleni ili mgeni akija atambue unawajibu gani kwa taifa,”ameebainisha.
Amesisitiza wahitimu hao kulinda uhuru na uchumi wan chi kama walivyo apa.
“Askari hawa wamefikia kiwango kinachokubarika katika jeshi la akiba na wapo tayari kutumikia taifa katika kutekeleza majukumu mbalimbali,”alieleza Kanali Kasyupa.
Katika mafunzo yao wahitimu hao walipata masomo mbalimbali kwa nadharia na vitendo, ikiwa ni pamoja na kwata, ukakamavu,mbinu za kivita, ujanja wa porini, usomaji ramani, huduma ya kwanza, zimamoto, uhamiaji, usalama wa taifa, Kuzuia na kupambana na rushwa , silaha ndogondogo, utimamu wa mwilki, uraia, kazi za polisi, uhamdisi wa medani,Sheria za Jeshi la Akiba, na vita vya msituni.
Katika risala yao wahitimu hao waliiomba serikali kuongeza bajeti ya mafunzo ya jeshi la akiba na kuwapa kipaumbele kujiunga na JKT na taasisi zingine za aserikali.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...