Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Dodoma
VIONGOZI wa Serikali pamoja viongozi wastaafu katika awamu tofauti leo wameungana na mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Rais Dk.Samia Suluhu Hassan wakati wa mkutano wa kampeni za uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29 mwaka huu.
Wakizungumza katika mkutano huo uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi and w Mkoa wa Dodoma wamewaomba wananchi kumchagua Rais Dk.Samia katika uchaguzi huo na ikifika Oktoba 29 waende kutiki kwa mgombea urais wa CCM.
Kwa upande wake Waziri Mkuu nstaafu Mzee John Samweli Malecela amesema Mkoa wa Dodoma umekuwa na historia tangu kuanzishwa mfumo wa vyama vingi kuongoza kwa idadi ya kura nyingi kwa wagombea Urais kupitia CCM kılıko mikoa yote.
Amesema huko nyuma ukienda kuangalia kwenye rekodi tangu Tanzania iwe huru kuchagua viongozi wake wa nchi ambaye ni Rais, kuna mikoa miwili ambayo imekuwa na rekodi nzuri tangu tuanze uchaguzi.
"Mikoa hiyo ni Iringa na Dodoma, sasa mimi nina jambo moja la kuwaomba Wanadodoma wenzangu, rekodi za huko nyuma zinaonyesha kila mara tumekuwa tukiwapa Marais wetu wagombea kura nyingi kuliko mikoa mingine.
“Sasa niwaombe safari hii ndugu zangu wote Mkoa wa Dodoma, nina uhakika wananchi wote tutampa kura zetu Dk. Samia," amesema na kutumia nafasi hiyo kumshuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ambaye amechaguliwa kugombea Urais kupitia CCM.
Kwa upande wake, Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango alifunguka namna ambavyo baadhi ya wananchi katika mataifa mbalimbali duniani wanavyotamani kuwa na kiongozi aina ya Dk. Samia.
"Kule unaponituma wenzetu wanatamani huyu awe Rais wao, nawasihi sana Oktoba 29 mwaka huu mkampigie kura Mama Samia mitano tena," alieleza huku wananchi wakiitikia mitano tena.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM, Dk. Bashiru Ali amesema kwamba nguvu ya CCM inatokana na umoja ndani ya Chama na ametumia nafasi kumpongeza Rais Dk. Samia kuliunganisha taifa.
"Nakushukuru Mwenyekiti kwa kuchukua kazi hii na umeisimamia kuunganisha vizuri nchi yetu inaendelea kufanya vizuri katika maeneo mengi, tupo kuwanadi wagombea kutokana wa ilani na utendaji wetu bora. Tunaomba muendelee kukiamini Chama Cha Mapinduzi na Dk. Samia," alisema.
Aidha ameahidi kuwa watafanya kazi ya kuomba kura katika ngazi zote kwa kuwaeleza wananchi ubora wa wagombea wa ngazi ya urais, Rais wa Zanzibar, wajumbe la baraza la wawakilishi, wabunge na madini.
Pia amesema watahakikisha wanatetea rekodi ya utendaji wa chama katika miaka mitano iliyopita, kazi tulizifanya na ahadi zilizotekelezwa na kufafanua yaliyomo ndani ya ilani ya uchaguzi ngazi ya taifa, mikoa na wilaya.
Wakati huo huo Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Bara, Mangula amesema wananchi wanapaswa kumpigia kura Rais Dk. Samia ili akamalize mazuri ambayo ameendelea kuyafanya kwa maslahi ya Watanzania.
"Ukiwa unaingia kwenye gari unatakiwa kuangalia anayekuendesha kwani wengine wanaweza kuwa 'malena' lakini ni tofauti kwa Rais Samia kwani ana leseni ya kimataifa inyoamfanya awe na uzoefu kuendesha nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...